ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 13, 2015

PRODUCER WA MO-MUSIC NA BARAKA DA PRINCE AACHIA NGOMA YAKE MPYA.

MTAYARISHAJI wa muziki  na mtunzi wa nyimbo kutoka studio za K-Records za jijini Mwanza Goodluck Gozbert aka 'Lollypop' ambaye ndiye mwandishi wa wimbo wa Mo Music Basi Nenda  na ule wa mpya wa Baraka Da Prince unaoitwa 'Siachani nawe' na nyingine nyingi, hatimaye ameamua kuchomoka kivyake kuonyesha umma kipaji alichonacho cha uimbaji kwa kufyatua mpini wenye hisia unaoitwa 'Acha waambiane'.

Akizungumza na GSengo Blog Lollypop amesema kuwa hii siyo track yake ya kwanza kuitoa hewani kwani muziki ndiyo chachu kwake kuwa  Mtayarishaji hii leo, akianzia kama mwimbaji wa muziki wa Injili kupitia kwaya kanisani, kundi na mwimbaji solo hatimaye hii leo Mtayarishaji mkubwa wa muziki tena wa kuaminika.

"Wimbo 'Acha waambiane' umebeba ujumbe wa kufariji wale wote wanaokutana na changamoto mbalimbali za maisha iwe ni kufukuzwa kazi, kukosa mtoto, changamoto za elimu, maradhi na kadhalika kiufupi wimbo unagusa kiroho zaidi" alisema Lollypop

Lollypop anawashukuru watanzania kwa kumpokea vyema katika Utayarishaji muziki kupitia nyimbo kadhaa zilizokubalika kitaifa na kimataifa zika-Hit zikiwemo zile alizo andika na hata kuwatayarishia wasanii wakali kama Baraka Da Prince na Mo Music, kwani zimempa kujiamini na changamoto zaidi ya kufanya makubwa katika fani.

BOFYA PLAY KUSIKILIZA SINGLE YAKE MPYA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.