Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akijadili na waandishi wa habari kuhusu promosheni ya Airtel yatosha zaidi wakati wa mkutano wa kuitambulisha promosheni hiyo kwa wakazi wa mkoa wa Dodoma |
Airtel Yatangaza kufanya droo ya wiki ya pili ya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza kufanya droo ya wiki ya pili ya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi siku ya kesho Ijumaa tarahe 13 februari 2015 ambapo washindi 7 wa gari aina ya Toyota IST watapatikana na kutangazwa
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kuitambulisha promosheni ya Airtel yatosha zaidi kwa wakazi wa Mkoa wa Dodoma, uliofanyika Dodoma Hoteli, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” kama ilivyo kawaida tunazunguka katika mikoa mbalimbali kutoa elimu juu ya huduma na bidhaa zetu pamoja na kuitambulisha promosheni hii ya Airtel Yatosha Zaidi tuliyoizindua hivi karibuni inayo wapa wateja wetu na watumiaji wa vifurushi vya Airtel yatosha nafasi ya kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku
Mpaka sasa tunao washindi watatu waliopatikana na Tayari wawili wamekabithiwa magari yao akiwemo Mwajuma Churian Mkazi wa Dar es saalam aliyekabithiwa gari lake siku ya Jumanne na leo Alhamisi tunakabithi gari kwa mwalimu mstaafu mkazi wa Mtwara Bwana Namtapika Kilumba . Mshindi wa tatu aliyetangazwa ni Bwana Ramadhani Dilunga ambaye ni Mkulima anatokea mkoa wa Pwani.
Nachukua fulsa hii kuwajulisha watanzania kuwa droo ya wiki ya pili ya promosheni hii inategemea kufanyika kesho siku ya Ijumaa ambapo washindi saba watapatikana na kutangazwa, tunaomba wateja wakae karibu na simu zao na watapigiwa simu za kutangiziwa ushindi huo toka namba 0684291105 ambapo Watanzania na wateja wetu 7 kesho wataondoka na Toyota IST.”
Napenda kutoa wito kwa wale ambao hawajajiunga na vifurushi hivi vya Airtel yatosha kufanya hivyo kwa kupiga *149*99# , au kununua vocha za Airtel yatosha au kununua vifurushi hivi kupitia huduma ya Airtel Money sasa. Kila mtanzania na mtumiaji wa huduma ya Airtel yatosha ataingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia hivyo ni wakati kwa wakazi wa Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania kuchangamkia fulsa hii. Aliongeza Matinde
Airtel Yatosha Zaidi ni promosheni iliyozinduliwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel mwanzoni mwa mwezi wa pili mpaka sasa watanzania wameendelea kubahatika kwa kujishindia magari aina yaToyota IST, promosheni hii itadumu kwa muda wa miezi miwili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.