ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 20, 2015

POLISI MWANZA WAMSAKA MTOTO ALBINO ALIYEPOTEA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola akionesha picha ya mtoto Pendo Emmanuel.
POLISI wametangaza kutoa dau la shilingi milioni tatu sawa na dola 1,700 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa mtoto albino, Pendo Emmanuel aliyetoweka nyumbani kwake na kupelekwa mahali pasipojulikana mwezi uliopita mkoani Mwanza.

Awali watu 15 walikamatwa na jeshi la Polisi mkoani Mwanza  kufuatia msako unaojulikana kama 'Hakuna kulala' dhidi mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) Pendo Emanuel kutekwa na watu wasiojulikana usiku  wa tarehe 27.12.2014 nyumbani kwao kijiji cha Ndami wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa hapa Valentino Mlowola amesema watu 8 kati ya 15 waliokamatwa awali wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi akiwemo baba  mzazi wa mtoto Pendo pamoja na kuipata pikipiki  inayosadikika kutumika katika tukio hilo.
Kamanda Valentino  mesema kuwa wengine 7 waliachiwa mara baada ya kukosekana ushahidi wa kuwatia hatiani. 
Mtoto Pendo Emanuel ni miongozni mwa albino 74 wanaoishi katika wilaya ya Kwimba na alikuwa namba 9 katika suala la kupatiwa ulinzi.
Takwimu zinaoyesha kuwa barani Afrika mtu mmoja kati ya  watu elfu 2000 huzaliwa akiwa na ulemavu wa ngozi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.