ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 20, 2015

KAGERA YAPOTEZA MCHEZO WAKE WA PILI NYUMBANI MBELE YA AZAM WANAONYAKUWA USHINDI WA PILI UGENINI

Kagera Sugar.
KAGERA SUGAR hii leo imepoteza mchezo wake wa pili mfululizo ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani CCM Kirumba Mwanza, mbele ya Mabingwa watetezi Azam Fc ambao wanaondoka sasa kanda ya ziwa wakiwa wamevuna pointi zote sita.
Azam Fc.
Waamuzi wa mchezo pamoja na ma-kapteini wa timu zote mbili.
Salaaam salaaam.
Benchi la Azam.
Benchi la Kagera Sugar.
Ilichukuwa dakika 3 tu za mchezo Azam Fc kupata bao....mfungaji ni Kipre Tchetche.
Azam wakishangilia goli la kwanza.
Mgeni rasmi wa mchezo Ligi kuu soka Tanzania Bara Kagera Sugar Vs Azam Fc, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (wa pili toka kushoto) akiwa ameketi meza moja na Mwenyekiti wa MZFA Jakson Songora (wa kwanza kushoto) na viongozi wengine.
Wadau wa soka na engo yao dimbani CCM Kirumba Mwanza. Dakika ya 38 Azam Fc wanapata bao la pili Didier kavumbagu akiunganisha krosi ya Kipre Tchetche, mabao yanayodumu hadi mapumziko. (0-2)
Kipindi cha pili Kagera Sugar wanazinduka toka usingizini na kunako dakika ya 55 wanapata bao mfungaji akiwa Rashid Mandawa.
Patashika ...
Mashabiki macho mchezoni....
Dakika ya 67 kona ya Brian  Majwega inatua kichwani mwa Didier kavumbagu anapiga free header na kusababisha maumivu mengine, hili ni bao la 3 kwa Azam.
Mabadiliko ya kipindi cha pili kwa Azam Fc kumtoa Didier Kavumbagu nafasi yake kuchukuliwa na Gaudance Mwaikimba naye Amri kiemba akiingia badala ya Kipre Tchetche, Himid Mao badala ya Frank Domayo.

Na yale ya Kagera Sugar, kwa mchezaji Pam Ngwai akiingia badala ya Babu Ali, Erick Kimanzi akiingia badala ya Shaimu mpala, Atupile Green akiingia badala ya Adam Kingwande, mabadiliko hayo hayakuleta tofauti yoyote kwani hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika Kagera Sugar 1, Azam 3. 
ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA KILICHOJIRI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.