ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 22, 2015

DK KEBWE AGIZA KIKAO CHA PAMOJA CHA WAMILIKI WA MADUKA YA DAWA NA MAMLAKA ZOTE HUSIKA KUFANYIKA JIJINI MWANZA JUMAMOSI HII

MWANZA.

MGOGORO uliopo wa wamiliki wa maduka ya dawa baada ya kufungiwa maduka yao wakati wa ukaguzi maalumu uliofanywa na kikosi kazi jijini Mwanza, umepelekea Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuagiza kufanyika kikao cha pamoja cha wadau wote husika ili kupata maelekezo ya serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, kwa Niaba ya Msajili wa Baraza la Famasi Tanzania, Nelson Njau, alisema kikao hicho cha pamoja kinachotarajiwa kufanika jijini hapa ni utekelezaji wa agizo la Wizara lililotolewa na Naibu Waziri, Dk Steven Kebwe, baada ya uongozi wa wamiliki wa maduka ya dawa mihimu kukutana naye kulalamikia zoezi lililokuwa likitekelezwa jijini Mwanza.

Njau alieleza kuwa kikao hicho kilichoagizwa na Naibu Waziri, Dk Kebwe kinachofanyika kesho (Jumamosi) jijini Mwanza katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Tanzania (BOT) tawi la Mwanza chini ya Mkuu ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii, Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza (RMO), Baraza la Famasi Tanzania.

Wengine watakaohudhulia kikao hicho ni pamoja na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), TRA, Manispaa ya Ilemela na Wamiliki wa maduka ya dawa Jiji na Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza ili vyombo hivyo muhimu kukutana na kuangalia jinsi ya wamiliki wa maduka ya dawa wanavyofanya shughuli za biashara hiyo.

“Kuangalia kama wanafuata taratibu na sheria zilizopo, kupata maelezo halali na ufananuzi wa Serikali ikiwa ni kutaka maduka yote ya dawa mhimu kutakiwa kubaki yabaki maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji kama sheria na kanuni zinavyoelekeza, lakini wanaotaka kubaki mjini kufuata taratibu kwa kuyapandisha hadhi maduka hayo ya dawa muhimu kuwa Famasi,”alisema.

Njau alisema kwamba biashara ya maduka ya dawa niya kitaalamu zaidi na kuhitaji udhibiti mkubwa na usimamizi wa karibu wa uwanzishwaji na uendeshwaji kutoka Mamlaka zote zinazohusika ikiwemo watoa huduma katika maduka ya dawa walio na sifa, vile vile kwenye majengo yaliyothibitishwa, kukidhi vigezo na kupatiwa usajili.

“Mamlaka zote zitasimamia hili, TFDA itasimamia ubora wa dawa , Barza la Famasi Tanzania litajikita katika udhibiti na usimamizi wa utowaji huduma za dawa pamoja na kusajili majengo, TRA itakuwa na jukumu la kukusanya kodi na Ofisi za Jiji, Manispaa na Halmashauri za Wilaya kuhakikisha zinatoa leseni za biashara huku Ofisi za waganga wakuu kudhibiti uzaji wa dawa za serikali,”alisisitiza.  

Wito wangu kwa wamiliki wa maduka ya dawa na wadau wengine kujitokeza kuhudhulia kikao hicho kilicho agizwa na Naibu Waziri Dk. Kebwe ili kupata maelekezo ya serikali na kuondoa mkanganyiko uliojitokeza wakati wa zoezi la ukaguzi, utambuzi na utekelezwaji wa kanuni na sheria zilizopo za kutoa huduma na biashara ya maduka ya dawa muhimu hapa nchini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.