ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, December 30, 2014

WATAKIWA KUJITOKEZA KUSHIRIKI BAHATI NASIBU YA COCA COLA MIKOA YA KANDA YA ZIWA

Mkuu wa Idara ya Mauzo wa Kampuni ya Nyanza Bottiling Ltd (NBCL), Japhet Kisusi akishuhudia tiketi ya mmoja wa washindi (katikati) ambaye ni msomaji wa Gazeti dada la michezi la Bingwa, wakati aliposhinda wakati wa kuchezeshwa droo ya tatu ya shindano la Coca Cola, kulia ni Afisa Mauzo wa NBCL akiakikisha tiketi hiyo kabla ya kumkabidhi zawadi ya  Kreti 10 za soda juzi jijini Mwanza. Picha Na Peter Fabian.
WANANCHI wa Mkoa wa Mwanza na Mikoa ya Kanda ya Ziwa, wametakiwa kushiriki michezo ya Bahati Nasibu itakayowawezesha kushinda kujinyakulia zawadi mbalimbali na kupata mitaji ya kujiendeleza katika sekta ya ujasiliamali.

Akizungumza katika shindano la tatu la kutafuta washindi la Coca Display Competion la Kampuni ya kutengeneza vinywaji baridi ya Nyanza Bottiling Ltd (NBCL), Mkuu wa Idara ya Mauzo ya Kampuni hiyo, Japhet Kisusi,    alisema wananchi wajitokeze kushiriki mashindano yanayoandaliwa na Kampuni hiyo.

“Ushiriki wao utawezesha kuwa washindi na kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo mamilioni ya fedha na vitu vya thamani na wakizitumia vyema zawadi katika kujiendeleza katika sekta ya ujasiliamali kutawezesha kujikwamua na umaskini na kujiongezea kipato,”alisisitiza.

Kisusi alisema kuwa katika shindano la tatu la wazi lililofanyika Desemba 29 mwaka huu katika ukumbi wa Makutano uliopo jijini Mwanza,    kumeshuhudia wateja 50 wa bidhaa za Kampuni ya NBCL wakikabidhiwa vyeti vya utambuzi na shukurani baada ya kununua Soda na kuzipanga kwa mpangilio kwenye Freji kama inavyoelekezwa na Maafisa mauzo kwenye Ofisi, Bar, Maduka, Hoteli, Hospitali na Migahawa.

“Tumeshuhudia mamia ya wateja waliohudhulia shindano hili la tatu wakiibuka washindi na kukabidhiwa zawadi ikiwemo ya TV Frati aina ya Sony iliyonyakuliwa na mshindi wa kwanza wa shindano hilo, Paul Alex, kutoka Bar ya Bariadi ya jijini Mwanza huku washindi wengine 21 wakinyakulia Kreti 10 za soda kila mmoja, saba wakipata saa za ukutani, watatu mipira ya miguu na sita wa vuvuzera,”alisema.

Naye Afisa Mauzo wa NBCL, Pramod Nair, alisema mbali na shindano hilo kumekuwa na idadi kubwa ya washiriki kujitokeza tofauti na mashindano yaliyopita kutokana na kuchezeshwa kwa uwazi na kutolewa zawadi kwa washindi, pia kushiriki na wateja katika chakula cha pamoja baada ya shindano na kubadilishana uzoefu na kufahamiana zaidi kwa wateja na Maafisa NBCL.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.