ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 12, 2014

WACHEZAJI WA KARETI, KICK-BOXING NA TAI-KWANDO WAFUNGULIWA CHUO JIJINI MWANZA

Mwalimu wa Kareti Albert Kisusi akitoa mafunzo ya mchezo huo kwa wanafunzi wake wenye umri kati ya miaka 7 hadi 10 katika maeneo ya Chuo cha Mashuati Atrs Club kilichofunguliwa hivi karibuni Isamilo jijini Mwanza.
Mwalimu wa Kareti Albert Kisusi akitoa mafunzo ya mchezo huo kwa wanafunzi wake wenye umri kati ya miaka 7 hadi 10 katika maeneo ya Chuo cha Mashuati Atrs Club kilichofunguliwa hivi karibuni Isamilo jijini Mwanza.
Mwalimu wa Kareti Albert Kisusi.
Mwalimu wa Kareti Albert Kisusi akitoa mafunzo ya mchezo huo kwa wanafunzi wake katika Chuo cha Mashuati Atrs Club kilichofunguliwa hivi karibuni jijini Mwanza. Picha Na Peter Fabian.
Mwalimu wa Kareti Albert Kisusi akitoa mafunzo ya mchezo huo kwa wanafunzi wake katika Chuo cha Mashuati Atrs Club kilichofunguliwa hivi karibuni jijini Mwanza.

NA PETER FABIAN, MWANZA.

CHUO cha mafunzo ya michezo ya Kareti, Kick-Boxing na Tai Kwando kimefunguliwa jijini Mwanza ili kuwezesha wachezaji kupata mafunzo na mbinu za mchezo huo kabla ya kushiriki mashindano mbalimbali ya ngazi ya Mkoa, Taifa na Kimataifa.

Mkurugenzi wa Chuo hicho cha Mashuati Arts Club, Mwl Albert Kisusi, alisema kuwa kuanzishwa kwa Chuo hicho kumelenga kuibua vipaji, kuwapa maarifa na mbinu wachezaji na kuwajengea uwezo na maumbo kabla ya kuingia kwenye mashindano ili kuwasaidia kufanya vyema.

“Chuo hiki tulichoanzisha na kukifungua hapa eneo la Isamilo Kata ya Isamilo Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, kimelenga zaidi kuwashirikisha watoto wa kuanzia umri wa miaka 5 hadi watu wazima wa umri usiozidi miaka 65 ambapo watakapojiunga walazimika kulipia ada ya kila mwezi ya Sh elfu arobaini na kupata mafunzo kwa hatua mbalimbali na kupatiwa vyeti baada ya kumaliza mafunzo kwa kila michezo na daraja,”alisema.

Kisusi alieleza kuwa wanafunzi na wachezaji watakaojiunga kwa michezo hiyo katika chuo hicho watatakiwa kufuata taratibu na miko na maadili ya michezo hiyo ili kuwawezesha kuwa wachezaji wazuri wenye umakini na maadili jambo ambalo limepewa kipaumbele kabla ya kujiunga na chuo hicho.

“Chuo hiki pia kitakuwa na sehemu maalumu ya mazoezi kwa watu wa kada mbalimbali ambapo wataweza kupunguza uzito, kufanya mazoezi ya GM, kupunguza tumbo kwa wanawake na wanaume kupunguza kitambi lakini kutakuwa na mafunzo ya Alob- Kings,”alisema.

Wito wangu kwa wananchi wa kutoka jiji la Mwanza na mikoa ya Kanda ya Ziwa na watakaopata nafasi ya kutembelea Chuo hiki watapata furusa ya kuona jinsi tulivyojipanga kutoa mafunzo hayo kwa kutumia walimu wazoefu na wenye uwezo wa kimataifa pamoja na kuwezesha wachezaji kuinua viwango vyao sanjari na kuendeleza vipaji vya wanafunzi.

Kisusi aliongeza kuwa Chuo chake kimekusudia kutoa walimu watakaokwenda kufundisha watu majumbani kwa makubaliano ambayo yatazingatia taratibu za Chuo ili kuwezesha kutoa mafunzo na kuongeza idadi ya wachezaji wa michezo hiyo pamoja na kuhamasisha kuanzishwa kwa Klabu mbalimbali ili kukuza michezo hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.