ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 13, 2014

TIMU YA POOL TAIFA YAJIWEKA SAWA KWA SAFARI ALL POOL CHAMPIONSHIP

Nahodha wa timu ya Taifa ya mchezo wa Safari Pool, Charles Venance akicheza wakti wa mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Kombaia ya Mkoa wa kimichezo wa Temeke uliochezwa katika Klabu ya Mpo Afrika Tandika mwishoni mwa wiki.Timu ya Taifa ilishinda 13-3.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Safari Pool wakiwa na viongozi wa Mkoa wa kimichezo mara baada ya timu ya Taifa kibuka na ushindi wa 13-3 dhidi ya timu ya kombania ya mkoa huo iliyochezwa mwishoni mwa wiki.

Na MwandishiWetu.
TIMU ya Taifa ya Safari Pool imeonyesha uwezo wa juu baada ya kuzichapa timu za kombania za Mikoa ya kimichezo ya Ilala na Temeke kwa siku tofauti katika kujiweka sawa na mshindano ya Afrika ya mchezo huo yajulikanayo kwa “Safari All Africa Pool Championship”.

Timu ya Safari Pool ilianza mchakato wakujipima ikiwa ni sehemu ya maandalizi na timu ya Kombania ya Mkoa wa kimichezo wa Ilala ambapo waliibuka naushindi wa 12-9 katika mchezo uliochezwa Ijumaa octoba 10,2014 kwenye Ukumbi wa Mashujaa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kutoka Ilala walikutana na timu ya Kombania ya Mkoa wa Temeke Jumamosi Octoba 11,2014 katika mchezo ulichezwa katika Ukumbi wa Mpo Afrika Tandika jijini Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa 13-3.

Timu ya Taifa ya Safari Pool ilimalizia ziara na Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni kkatika mchezo uliochezwa kwenye Ukumbi wa Face to Face 0ctoba 12,2014 ambapo pia timu yaTaifa iliibuka na ushindi wa michezo 13-7.

Akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa timu ya Taifa, Denis Rungu alisema kikosi chake kikosafi na mchakato wa mechi za kirafiki tatu za mikoa ya kimichezo ya Ilala, Temeke na Kinondoni ni sehemu ya kupima kikosi chake lakini pia ni sehemu ya mchujo wa kupata wachezaji 8 kutoka kundi la wachezaji 16 walioko timu yaTaifa.

Alisema Kocha timu tayari imeshaingia kambini toka jana ambapo ndio sehemu muafaka ya kujiandaa vema na mashindano ya Afrika kwa mwaka 2014 ambapo Tanzania ndio muandaaji.

Mashindano ya Safari All Africa Pool Champonship yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Octoba 16 na kumalizika Octoba 18 ambapo mgeni rasmi anayetarajiwa kufungua mashindano hayo ni Waziri wa Habari Utamaduni, Vijana na Michezo.


Nchi zilizothibitisha kushiri kampaka sasa ni mabingwa watetezi Zambia, Afrka Kusini, Kenya, Cameroon, Lesotho, Malawi, Uganda na wenyeji Tanzania.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.