ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 13, 2014

HOSPTIALI ZA WILAYA ZA MISUNGWI, SENGEREMA, MAGU NA KWIMBA ZAPEWA VIFAA VYA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 68


TAASISI ya Afrika ya Brien Holden Vision Institute (BHVI) imezipiga jeki ya vifaa tiba vyenye thamani ya Sh milioni 68 ili kukabiliana na tatizo la wagonjwa wa macho katika Hosptali za Wilaya ya Misungwi na Sengerema, Magu na Kwimba mkoani Mwanza.

Msaada huo ulikabidhiwa mwishoni mwa juma lililopita na Meneja Mipango wa BHVI Afrika, Mary Wepo kwenye hafla fupi iliyofanyika ofisi za Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza chini ya ufadhili wa Stanard Chartered Bank Tanzania Ltd kupitia mpango wa miaka minne wa Afrika Pubilic Health Division unaotekelezwa katika mikoa ya Mwanza na Mbeya hapa nchini.

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo, Wepo alisema kutokana na kuwepo tatizo hilo la watu kushindwa kuona vizuri Taasisi yake iliamua kufanya utafiti na hatimae kubaini kuwepo tatizo hilo katika mikoa ya Mwanza na Mbeya ambapo imeanza kutekeleza mpango tiba chini ya ufadhili wa Standard Chartered hapa nchini.



“Tumekabidhi mashine ya kupimia macho, flemu za miwani, lenzi za macho,vioo, mashine ya kuchongea na vifaa vidogovidogo pamoja na dawa ambavyo ni kwa ajili ya tiba na tatizo la wagonjwa wa macho watakaofika kupata huduma kwenye Hospitali za Wilaya hizo na Vituo vya Afya,”alisema.

Naye Mwakilishi Mkazi wa BHVI nchini, Eden Mashayo,  alisema mpango huu Mkoa wa Mwanza unatekelezwa katika Hospitali za Wilaya za Misungwi, Sengerema, Magu na Kwimba amapo katika Mkoa wa Mbeya ni Hospitali za Wilaya Mbozi, Ileje, Kyela, Mbeya Mjini na Rungwe.

“Tumedhamilia kupunguza na kulishughulikia tatizo hili la wagonjwa wa macho ambalo limeonekana kuanza kushika kasi kwa watoto na wawanafunzi wa shule za masingi, sekondari na vyuo mbalimbali hapa nchini na katika maeneo hayo ambapo pia watatembelea Wilaya hizo kuweka kambi za tiba kwa wagonjwa na kuendelea kutoa elimu na mafunzo kwa wataalamu,”alisema.

 Mashayo alisema katika shule za msingi wamekwisha toa mafunzo kwa walimu wa afya wawali za wilaya hizo ili kuwawezesha kuwatambua wanafunzi walio na tatizo la macho wakati watakapolalamika kutoona vizuri ambapo watwezesha kuwafikisha kwenye Vituo vya Afya na Hospitali kupata huduma.

Kwa upande wake Meneja wa Standard Chartered Bank tawi la Mwanza kwa niaba ya Makao Makuu, Shufaa Salum, alisema Benki hiyo imekuwa ikifadhili mpango huo kwa miaka mnne hapa nchini katika mikoa hiyo miwili kwa Hospitali za Wilaya na Vituo vya Afya kwa gharama ya USD milioni 58 kwa kipindi chote.

“Tukiwa wadau kwa jamii tuliguswa na tatizo hili ambalo limekuwa likiikumba jamii hivyo kupelekea uamuzi wa kutoa kiasi hicho cha fedha hizo zitakazotumika kununulia vifaa tiba kwa wagonjwa wa macho kwa miaka minne kwa Mikoa miwili ya Mbeya na Mwanza hapa nchini ambapo kila Wilaya itapata vifa vyenye thamani ya Sh milioni 17.563,000 kila moja,”alisema.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Dr Valentino Bangi, akipokea vifaa hivyo. alipongeza Taasisi hiyo ya BHVI na Benki ya Standard Chartered kwa msaada huo ambao utasaidia wagonjwa wa macho kupata tiba na huduma ya vifaa vitakavyo wawezesha kuona na kusomea, pia amewataka vifaa hivyo kutumika kama ilivyokusudiwa kwa kulenga kukabiliana na tatizo la wagonjwa wa macho.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.