Kileleni yaonekana Hospitali ya Rufaa ya Bugando. |
NA PETER FABIAN, MWANZA.
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza imemuagiza Dalali wa Makakama hiyo, Kampuni ya Katengeza Court Broker ya jijini Mwanza, kuyakamata na kuyapiga mnada magari manane mali za Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) ya jijini hapa.
Hatua hiyo ya utekelezaji wa amuri halali wa Mahakama hiyo, kufatia kesi za watumishi 36 wa BMC kufungua kesi ya madai katika Mahakama hiyo, na kutolewa uamuzi kutokana na taratibu na sheria za kufukuzwa kazi kwa watumishi ambao walikuwa ni walinzi kutokana na kukiukwa kwa taritibu na sheria na uongozi wa Hospitali ya BMC na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Katika kesi hiyo ya madai namba 4 ya mwaka 2004, walinzi hao wakiongozwa na mwenzao Raphael Alberto, walifungua kesi dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji wa BMC (wakati huo Dk Charles Majinge), Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakipinga kuachishwa kazi bila kufuata utaratibu.
Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Aisheri Sumari, Aprili 11/2013 na Septemba 11/2013 baada ya kusikilizwa kwa makundi mawili kutokana na wadaiwa kuwa tofauti (yaani BMC, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Mwanasheria Mkuu).
Kufatia hukumu hiyo, ilionekana walinzi 36 waliachishwa kazi kinyume cha sheria na hivyo kuamua waendelee kuhesabiwa kama watumishi wa Hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki na kuendeshwa kwa pamoja na serikali.
Kwa mujibu wa hukumu hiyo, Mahakama iliamua mlalamikaji wa kwanza hadi wa 18 waliokuwa wameajiriwa na BMC, kila mmoja alipwe sh Milioni 5 kama gharama za usumbufu wa kuachishwa kazi (BM ilipe sh M 90).
Huku kuanzia mlalamikaji wa 18 hadi wa 36 walioajiriwa na serikali, nao iliamuliwa kila mmoja alipwe kiasi hicho hicho sh milion 5 (Katibu wa Wiazara na Mwanasheria nao sh Milioni 90) na hivyo jumla kutakiwa walipwe sh milioni 180.
Kufatia maamzi hayo, ili waajiriwa wa BMC walipwe mafao yao, mahakama imetoa amri ya kukamata magari manane ya Hospitali hiyo liwemo linalotumiwa na Kaimu Mkurugenzi wa MBC na lile la kubebea wagonjwa (Ambulance).
Katika hati ya dalali inaonyesha magari yanayotakiwa kukamatwa na namba zake kama yalivyo ainishwa kwenye amri hiyo ni T. 654 AFM aina ya Nissan Patrol, T. 668 AFM aina ya Toyota Land Cruiser, T. 676 AFM, T. 698 AFM, T. 480 AMS, T. 848 AWN, T. 702 AFM na T. 723 AFM.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Udalali, Celestine Katengeza, jana alisema kwamba siku yoyote atatekeleza amri hiyo halali kutokana na muda wa Notisi aliyotoa kuisha ya siku 30 kwa uongozi wa BMC (ambao ulitolewa kutoka Agost 20 hadi Septemba 20 mwaka huu) kumalizika bila kulipa kiasi hicho cha sh milioni 90 za watumishi hao.
Wagonjwa mahututi hutegemea usafiri wa ambulance kusafirishwa toka eneo moja hadi kufika hapa kwaajili ya matibabu zaidi. |
“Nisipotekeleza zoezi hilo nitakuwa nakiuka amri halali ya Mahakama hivyo wakati na siku yoyote nitaitekeleza.” Alidai Mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa wakati akitoa notsi hiyo aliambatanisha fomu ya amri ya kuzuia magari hayo yasisafiri kwenda nje ya eneo la BMC (Prohibitory Order).
“Magari hayo ikiwemo Ambulance na linalotumiwa na kaimu Mkurugenzi Dk Profesa Giryoma, hayatakiwi kuondolewa ndani ya eneo la Hospitali, atakaye yaondoa atashitakiwa kwa kuzuia utekelezaji wa amri halali ya mahakama.” Alidai Katengeza.
Dalali huyo alieleza, baada ya zoezi la kukamata mali za wadaiwa wa kwanza (BMC), Mahakama itaelekeza amri ya kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mwanasheria Mkuu wa serikali walipeje kiasi kiasi cha sh M 90 wanachodaiwa.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa BMC, Profesa Giryoma, akizungumza kwa njia ya simu ya mkononi alikiri kukabiliwa na amri hiyo kufuatia hukumu ya kesi ya madai namba 4/2010 iliyotolewa mwaka jana na Mahakama hiyo.
Prof Giryoma alieleza kuwa baada ya kuamriwa wamekuwa wakitafuta fedha za kulipa ili kuepusha mali hizo zisikamatwe na kuuzwa kwa mnada jambo ambalo linaweza kukwamisha utendaji na huduma kwa wagonjwa wa BMC.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.