ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 9, 2014

MWENGE WA UHURU WAPOKEWA NA MIRADI YA NGUVU WILAYANI RORYA

Kijiji cha Ikoma ndiyo kunako lango kuu la mpakani mwa wilaya ya Rorya na wilaya ya Tarime mkoani mara ambapo Mwenge wa Uhuru  ulipokelewa hapa ukitokea wilayani Tarime ambapo pamoja na kukagua pia ulizindua miradi mbalimbali ya shughuli za maendeleo. 
Mkuu wa wilaya ya Tarime John Henjewele (kushoto) akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa mkuu wa wilaya ya Rorya Elias Goroi (kulia) ili upate kukimbizwa katika vijiji mbalimbali wilayani humo kukagua miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo, kulia kabisa ni moja ya makamanda viongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Hamza Ibrahim Mohamed.
Maskauti wa wilaya ya Rorya wakiulaki Mwenge wa Uhuru.
Mkuu wa wilaya ya Tarime John Henjewele (mwenye karatasi nyeupe katikati) akiongoza mchakamchaka wa makamanda na wadau wake kwenda kuukabidhi mwenge wa uhuru kwa wananchi wa Rorya, uliobebwa na Lt. Tunu Oscar Mlowezi
Mkuu wa wilaya ya Tarime John Henjewele akitoa tamko lamakabidhiano ya Mwenge wa Uhuru unaokimbizwa wilaya hadi wilaya, mkoa hadi mkoa hapa nchini. 
Mwenge wa Uhuru ukimulika.
Shughuli zilizoandaliwa mwaka huu wilayani Rorya kupitia kazi nzuri inayofanywa na mbunge wake Mhe. Lameck Airo, zimezingatia kwa makini vipaumbele vya mikakati ya masuala muhimu kama vile; Mchakato wa kupatikana Katiba mpya, Mapambano dhidi ya UKIMWI, Malaria, Rushwa na Madawa ya kulevya.
Safu ya Viongozi  wa Rorya ikiwa imeambatana na wananchi wake kuupokea Mwenge wa Uhuru.
Wacha furaha itawale "Fagilia Kizanzibari......Halua halua"
Wananchi wa kata ya Ikoma wilayani Rorya sanjari na watoto wao wakiweka historia kushuhudia mbio za Mwenge wa Uhuru 2014.
Shughuli za makabidhiano zikiendelea.
Watoto wanavituko..... Hapa alijitokeza bodaboda 'spesheli' akiwa na usafiri wake.
Kusanyikoni.
Kwa umakini na utulivu.
Tarime to Rorya.
"Pamoja na vipaumbele hivyo,pia Mwenge wa Uhuru utapata nafasi ya kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kukagua miradi ya maendeleo ya Kisekta kama vile nyumba za watumishi, hosteli za wanafunzi, kituo cha kilimo/ugani, wodi ya wakina mama na watoto na barabara na kadhalika" Ilisema taarifa ya mkuu wa wilaya ya Rorya Mhe. Elias Goroi.
Miradi itakayo husika mwaka huu ina jumla ya shilingi za Tanzania 963,038,170.00 ambazo ni michango ya Halmashauri ni Tshs 140,838,520.00, michango ya wananchi ni Tsh 27,307,650.00 na michango ya wahisani ni Tshs 794,892,000.00.
Wengine walidiriki kukweamiti ili kulishuhudia tukio.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2014 Rachel Stephen Kassanda akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba ya watumishi katika kata ya Ikoma tarafa ya Girango wilayani Rorya mkoani Mara. 
WANANCHI wa kata ya Ikoma tarafa ya Girango wilayani Rorya wameaswa kutokata tamaa kwa kazi nzuri ya kuchangia miradi ya maendeleo.

Hayo yalisemwa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,Rachel Kasanda wakati akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba ya watumishi. "Hongereni kwa kazi nzuri mliyoifanya  na  ninawaasa msikate tamaa endeleeni kuchangia miradi ya maendeleo katika maeneo yenu".alisema kasanda.

Kasanda alisema kuwa ni jambo la kujivunia kwa kazi kubwa iliyofanywa na wananchi wa  Ikoma kwa kuchangia kiasi cha Sh.milion 11.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2014 Rachel Stephen Kassanda akifanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba ya watumishi katika kata ya Ikoma tarafa ya Girango wilayani Rorya mkoani Mara. 
Akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa nyumba za watumishi mkuu wa shule ya msingi Bugiri,Jackson Nyangubo alisema kuwa anaishukuru halmashauri kwa kuwachangia Sh.Milion ishirini. "Sisi wananchi tumechangia Sh. Milion 11 lakini tunaishukuru serikali kwa kutuchangia Sh milion 20 na tuanaamini kuwa jengo hili litakamilika mapema".alisema. Nyangubo.

Mwenge wa Uhuru uliwasili waliyani hapa juzi ukitokea wilaya jirani ya Tarime na kuzindua pamoja na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo jengo la bweni la wasichana shule ya sekondari Roche, mtandao wa vikundi vya wakulima na wafugaji (MVIWANYA)  na kukagua kikundi cha watu wanaoishi na virusi vya ukimwi(WAVIU).

Upande wa nyuma hii ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa nyumba ya watumishi katika kata ya Ikoma tarafa ya Girango wilayani Rorya mkoani Mara. 
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2014 Rachel Stephen Kassanda akizungumza na wananchi wa kata ya Ikoma mara baada ya kufanya ukaguzi na hatimaye kuweka jiwe la msingi  mradi wa ujenzi wa nyumba ya watumishi.
Makaribisho tukioni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.