Taasisi ya RafikiElimu FOUNDATION kupitia MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINJI inatangaza nafasi za MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA MASHINE ZA KUTOTOLEA VIFARANGA WA KUKU.
Mashine zitakazo fundishwa kutengeneza ni INCUBATOR (MANUAL & AUTOMATIC) ZENYE UWEZO WA KUTUNZA JOTO KWA SAA 48 PAMOJA NA KUTOTORESHA MAYAI KUANZIA 240 HADI 5000.
ADA YA MAFUNZO :
Ada ya mafunzo haya ni SHILINGI LAKI MBILI NA ELFU HAMSINI TU (Tshs. 250,000/=) na inalipwa kwa awamu mbili.
TAREHE YA KUANZA KWA MAFUNZO
Mafunzo haya yatafanyika kwa muda mwezi mmoja kuanzia tarehe 06 OKTOBA 2014 hadi tarehe 10 NOVEMBA 2014.
FOMU ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO :
Fomu za kujiunga na mafunzo haya zinapatikana ofisini kwetu kwa gharama ya SHILINGI ELFU KUMI NA TANO TU
(Tshs.15,000/=).
MWISHO WA KUCHUKUA FOMU :
Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30 SEPTEMBA 2014.
Ofisi zetu zinapatikana katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU.
JINSI YA KUFIKA OFISINI KWETU:
Kufika ofisini kwetu, panda daladala za UBUNGO- CHANGANYIKENI kisha shuka kituo cha TAKWIMU halafu tembea hatua ishirini mbele kisha tazama upande wako wa kulia utaona ofisi imeandikwa RAEFO TANZANIA.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu 0784406508.
KWA WAOMBAJI WALIOPO NJE YA MKOA WA DAR ES SALAAM:
Kwa waombaji waliopo nje ya mkoa wa Dar Es salaam,, mafunzo yatatolewa kwa njia ya posta.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI KWA WAOMBAJI WALIOPO NJE YA MKOA WA DAR ES SALAAM.
Kwa waombaji waliopo nje ya mkoa wa Dar Es salaam, watatumiwa fomu za kujiunga na mafunzo haya kwa njia ya barua pepe. Tuma barua pepe ya maombi ya fomu ya kujiunga na mafunzo haya kupitia barua pepe yetu ambayo ni : rafikielimutanzania@gmail.com .
Maombi yako yaelekezwe kwa Mkurugenzi Mtendaji, RafikiElimu Foundation.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.