ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 19, 2014

TCCIA MWANZA HAIUNGI MKONO MGOMO WA KESHO WA UMOJA WA WAFANYABIASHARA MKOA WA MWANZA.

Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara  wenye viwanda na wakulima Mkoa wa Mwanza, Leopord Lema (kulia).
NA ALBERT G. SENGO MWANZA
Wakati wafanyabiashara mkoa wa Mwanza wakiwa  wametangaza mgomo wa kutofungua maduka yao kuanzia  kesho kwa siku zisizojulikana kwa kile walichodai Mkurugenzi wa jiji hilo, Hassan Hida kukataa kukutana nao kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili.

Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara  wenye viwanda na wakulima Mkoa wa Mwanza, Leopord Lema amesema TCCIA haiungi mkono mgomo huo uliopewa baraka na Umoja wa wafanyabiashara mkoa kwani haioni mgomo huo kuwa na sababu za msingi na wala hauna tija kwa maendeleo ya jiji la Mwanza.

Lema ameongeza kuwa mambo yote ya malalamiko ya Umoja wa wafanyabiashara hao yalikwisha wasilishwa kwenye vyombo husika na ofisi ya TCCIA Mwanza baadhi yake yakitolewa ufafanuzi na utekelezaji huku mengine yakisubiri maamuzi rasmi. BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAMKO.
Kama mgomo huo utafanikiwa utakuwa wa pili kufanyika baada ya mara ya kwanza kutokea kati ya Desemba mwaka jana hadi Januari mwaka huu wakati wafanyabiashara hao wakigomea matumizi ya  mashine za Stakabadhi za Elekitroniki (EFD) na kusababisha kero kubwa wa wananchi.

Hata hivyo mgomo wa kesho hauhusishi tena mashine za EFD badala yake umejikita katika matatizo yanayowakabili ambayo ongezeko la kodi ya taka kutoka Sh 8,000 hadi 10,000, kutoza fedha za kuweka bidhaa zao nje ya duka na mambo mengine ya kukamatiwa mali zao.

Uamuzi huo ulifikiwa jana katika mkutano mkuu ulioitishwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), mkoa wa Mwanza kwa lengo la kutoa taarifa za mazungumzo kati ya Serikali  juu ya matumizi ya mashine za EFD.

Kabla ya kufikia azimio la kutofungua maduka yao, Mwenyekiti wa JWT, mkoa wa Mwanza, Christopher Wambura aliwaeleza wafanyabiashara hao jitihada alizofanya za kukutana na mkurugenzi huyo lakini mara zote ziligonga mwamba.

Kwa upande wa Meneja wa TRA mkoa wa Mwanza, Jeremia Lusana amesema kitendo cha cha wafanyabiashara hao kugoma kinasabaisha hasara kubwa katika suala la mapato huku akitishia kuwafungia lenseni za biashara zao.

Naye Kamanda wa Polisi Mwanza, Valentino Mlowola amesema askari wake watakuwa tayari kuimarisha ulinzi kwa siku ya kesho ikiwa kutakuwapo na hali ya uvunjifu wa amani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.