Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa 11 wa Sekta ndogo ya Pamba Kanda ya Magharibi mikoa inayolima zao hilo, katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Tawi la Mwanza. |
Mkutano wa 11 wa Sekta ndogo ya Pamba Kanda ya Magharibi mikoa inayolima zao hilo, katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Tawi la Mwanza. |
Wajumbe toka mikoa na mikoa, wilaya na wilaya. |
Sekretarieti ya Mkutano wa 11 wa Sekta ndogo ya Pamba Kanda ya Magharibi mikoa inayolima zao hilo, katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Tawi la Mwanza. |
Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Dr. Festus Limbu ambaye ni Mbunge wa jimbo la Magu (wa pili kutoka kushoto) akiwa na wadau wa Sekta ya Pamba. |
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (kushoto) akiwa na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo wakijadili masuala kadhaa. |
Wadau wa Pamba. |
NA PETER FABIAN, MWANZA.
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Injinia
Christopher Chiza, ameiagiza Menejimenti ya Bodi ya Pamba kuwachukulia hatua
kali Makamupuni ya ununuzi wa Pamba yaliyofanya uchakachuaji wa minzani wakati
wa ununuzi wa pamba musimu wa 2014/2015.
Pia ameliagiza Shirika la Viwango (TBS) pamoja
na Wakala wa Vipimo Tanzania kuwakamata na kuwafikisha mahakamani, wanunuzi wa
zao la pamba wanaochakachua mizani kisha kuwaibia kilo wakulima wa pamba.
Waziri Chiza aliyasema hayo jana alipokuwa
akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 11 wa wadau wa Sekta ndogo ya Pamba,
uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Mwanza kisha
kuhudhuriwa na wakuu wa wilaya, wabunge, wakurugenzi na wenyeviti wa
halmashauri na wadau wengine.
Alisema TBS pamoja na Wakala wa Vipimo
nchini wanao wajibu wa kuwakamata na kuwafungulia mashtaka wafanyabiashara wote
wa zao la pamba wanaotumia mizani mibovu, na kwamba huo ni wizi usiovumiliwa na
serikali.
Waziri Chiza alisema kumekuwepo na tabia chafu
ya wanunuzi wa pamba kuwaibia wakulima, rasilimali yao hiyo kinyume cha sheria,
na kwamba la kudhibiti wizi huo hawezi kulifanya yeye kama waziri bali mamlaka
husika za Wakala wa Vipimo na TBS.
“Wengine wananipigia simu mimi ili nidhibiti
mizani iliyochakachuliwa, kimsingi mimi ni kiongozi wa juu siwezi kufanya
hivyo, wapo TBS na Wakala wa Vipimo ambao ndiyo wenye mamlaka ya kudili na watu
kama hawa.
“Lakini pia nakiri kwamba serikali haijawahi
kuchangia fedha kwenye mfuko wa kuendeleza zao la pamba, ingawa ni mdau mkubwa
wa sekta hii. Kwa hiyo serikali inaiagiza Bodi ya Pamba ihakikishe tatizo la
mbegu za pamba zisizoota lisijitokeze tena,” alisema Waziri huyo wa Kilimo,
Chakula na Ushirika.
Katika hatua nyingine, waziri huyo alisema
serikali inaandaa utaratibu wa kuanza kuwalipa fidia wakulima walioathirika na
mbegu za pamba ambazo hazikuota kwenye mashamba yao, licha ya kuuziwa na wadau.
Kuhusu kuvunjwa kwa uongozi wa Bodi ya Pamba,
Waziri Chiza, alisema serikali kupitia wizara yake ipo kwenye mchakato maalumu
wa kuhakikisha viongozi wengine wapya wa bodi hiyo wanapatikana, kwa lengo la
kusimamia Sekta ndogo ya Pamba.
“Naomba niweke kumbukumbu sawa katika mkutano
huu ambao upo kisheria. Bodi ya Pamba imeshamaliza muda wake, na wizara yangu
inafanya mchakato wa kupata viongozi wengine kwa ajili ya kusimamia Sekta ndogo
ya Pamba,” alisema Waziri Chiza.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa muda wa mkutano
huo wa wadau wa zao la pamba, Dk. Limbu alisema Bodi hiyo ya Pamba inakabiliwa
na ukata mkubwa wa fedha za uendeshaji wa sekta hiyo ndogo kwa wakulima kote
nchini kutokana na serikali kutwasilisha mchango wake katika Mfuko wa
kuendeleza zao la Pamba (CTDF) kwa wakati.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Injinia Evarist
Ndikilo aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo wa 11 wa Sekta ndogo ya Pamba kwamba,
mkoa huo unashika nafasi ya pili kitaifa kwa kulima zao la pamba ukiongozwa na
Mkoa wa Simiyu, hivyo aliomba zao hilo litiliwe mkazo ili kuleta maendeleo kwa
jamii.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.