Hizi ndizo zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa Fainali za mashindano ya ngoma za asili mikoa ya Kanda ya Ziwa zinazofanyika leo viwanja ya Polisi mabatini jijini Mwanza. Peter Fabian. |
NA PETER FABIAN, MWANZA.
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola mgeni rasmi Fainali za mashindano ya ngoma za asili mikoa ya Kanda ya Ziwa yanayofanyika leo Jumamosi jijini Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Kampuni ya Tanzania Braweries Ltd (TBL) Meneja wa Bia ya Balimi Extra, Edith Bebwa, alisema mashindano ya mwaka huu ya ngoma za asili mikoa ya Kanda ya Ziwa yanafikia kilele leo Agosti 16 katika viwanja vya Polisi Mabatini jijini hapa.
Bebwa alieleza kwamba mashindano hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka kwa lengo la kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania ikimulika zaidi Kanda ya Ziwa na yamekuwa yakidhaminiwa na TBLb kupitia bia ya Balimi Extra.
“Tunawakaribisha wananchi katika kushuhudia fainali hizi katika viwanja vya Polisi Mabatini ili kuwapa moyo washindani lakini pia kujionea vikundi hivyo vya utamaduni vikichuana ili kumpata mshindi wa mwaka huu, huku walengwa wakubwa wakiwa waliotimiza miaka 18 na kuendelea,”alisema.
Meneja huyo alizitaja zawadi kwa washindi ambapo mshindi wa kwanza (bingwa) atajinyakulia kiasi cha Sh milioni 1.1, kombe na medali za dhahabu, mshindi wa pili atapata Sh 850,000., mshindi wa tatu atapata Sh 600.000., mshindi wan ne atapata Sh 500,000 na mshindi wa tano hadi wa kumi kila mmoja tapata kifutajasho kiasi cha Sh 250.000 kwa mwaka huu.
Naye Meneja wa Matukio Kanda wa TBL, Erick Mwayela alivitaja vikundi vya utamaduni vilivyoingia fainali na mikoa vinakotoka kwenye mabano kuwa ni Magereza na Bugobogobo (Tabora), Mabuli ya jeshi na Wanunguli Bugumbagu (Shinyanga), Rugu Karagwe na Rugoroile (Kagera), Mwanalyaku Magu (bingwa mtetezi) na Bujora (Mwanza) na Kiwajaki Group na Musoma One (Mara).
Wito kwa majaji wa mashindano hayo ni kuzingatia kanuni za mashindano ambazo alizitaja kuwa ni vikundi kuimba wimbo mmoja wa asili, wimbo wa bia ya Balimi, utumiaji vyombo vya asili na ubunifu jukwani pamoja na uchangamfu wa vikundi vinapotoa burudani ili kumpata mshindi aliyekidhi vigezo hivyo jambo ambalo litaondoa malalamiko.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.