ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, August 3, 2014

MKOA WA MWANZA WAANZA RASMI KUSAKA VIJANA U17 WATAKAO WAKILISHI MKOA KATIKA MASHINDANO YA KITAIFA YA AIRTEL RISING STARS.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akipiga penati kuashiria uzinduzi wa Airtel Rising Stars mkoani hapa.
Katibu wa Chama Cha Soka mkoa wa Mwanza MZFA Nasibu Mabrouk akizungumza na wadau wa soka, wachezaji na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa ligi ndogo itakayoshirikisha timu tatu kusaka vijana 18 watakaounda timu ya mkoa.



Anaye zungumza ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula.

MICHUANO ya Airtel Rising Star imeanza rasmi kutimua vumbi hapa jijini Mwanza.

Ndani ya dimba la CCM Kirumba Mwanza timu ya vijana wa kituo cha elimu na vipaji cha Alliance Academy wameanza vyema michuano hiyo kwa kuicharaza TSC Academy bao 4-2.

Jumla ya timu tatu kutoka vituo vitatu vya soka mkoani Mwanza, zinashiriki michuano hiyo ambapo wataalamu wanne waliochaguliwa na Chama cha soka mkoa wa Mwanza MZFA wanasimamia zoezi la kupata wachezaji 18 U17 watakao uwakilisha mkoa kwenye mashindano ya Airtel Rising Stars yatakayofanyika baadaye kitaifa jijini Dar es salaam. 

Mbali na Alliance pamoja na TSC kituo kingine ni Misungwi Academy.

Akizugumza kuzindua mashindano hayo Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula yeye amesema kuwa hakuna timu bora duniani iliyomea na kupata mafanikio kimataifa bila kuweka msingi kwa timu za vijana. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Sehemu ya wachezaji washiriki wa Airtel Rising Stars na waandishi wa Habari.
Wakiwa katika uzi wao mweupe TSC Academy (wanaonekana kwa ukaribu zaidi) wakisikiliza shughuli ya ufunguzi wa Michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Mwanza.
Airtel.
Walioketi mbele ni wakufunzi wa soka walioteuliwa na MZFA kuvibaini vipaji vya soka kwaajili ya uteuzi wa timu ya mkoa wa Mwanza Airtel Rising Stars.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akitambulishwa na nahodha wachezaji wa timu ya vijana toka TSC Academy kabla ya filimbi kupulizwa kuashiria uzinduzi wa Airtel Rising Stars ndani ya dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akitambulishwa na nahodha wachezaji wa timu ya vijana toka Alliance Academy kabla ya filimbi kupulizwa kuashiria uzinduzi wa Airtel Rising Stars ndani ya dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akitambulishwa na nahodha wachezaji wa timu ya vijana toka Alliance Academy kabla ya filimbi kupulizwa kuashiria uzinduzi wa Airtel Rising Stars ndani ya dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.
Nahodha wachezaji wa timu za vijana toka Alliance Academy(L) na TSC Academy (R) katika picha ya pamoja na waamuzi wa mchezo huo, kabla ya filimbi kupulizwa kuashiria uzinduzi wa Airtel Rising Stars ndani ya dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.
Alliance Academy.
TSC Academy.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.