ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 10, 2014

MGANGA WA JADI NA MFUASI WAKE WAFARIKI BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI WAKICHIMBA DHAHABU KATIKA ENEO LA WAPONDA KOKOTO.

WATU wawili wamefariki baada ya fukiwa na kifusi ndani ya shimo walilokuwa wakichimba dhahabu eneo la Kangaye ‘A’Wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Christopher Fuime amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa tayari kikosi cha uokoaji kimeisha pata maiti mmoja kutoka kwenye eneo la tukio na kazi inaendelea ya kutafuta maiti nyingine ambayo bado haijapatikana . 

“Waliokufa ni Mganga wa jadi na mfuasi wake wamefariki dunia katika shimo walilokuwa wakidai wanachimba dhahabu baada ya kukosa hewa ndani ya shimo hilo kutokana na kuporomokewa na kifusi. 

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa kikosi cha Ukoaji jijini hapa Ispector Augustino Magere alieleza kuwa tukio hilo la lilitokea juzi (siku ya jumanne 8/july2014) majira ya saa 6 mchana katika kata ya Nyakato ambapo alipata taarifa kutoka eneo la tukio ili kufanya ukozi wa miili iliyokuwemo ndani ya shimo.

Magere aliwataja marehemu kuwa ni Sophiani Hamisi (60) mkazi wa Kangaye pamoja na Zuberi Kaima (45) mkazi wa Nyakato ambapo ilidaiwa na Sophiani kuwa eneo hilo alioteshwa lina dhahabu zilizoachwa na wakoloni.

“Eneo hili linalosadikika kuwa na dhahabu lilizuiliwa kutokana na kwamba ni eneo hatari kwa maisha ya binadamu na wala halistahili kuchimbwa” alisema.
Pia aliongeza watu hao walikufa kwa kukosa hewa kutokana na shimo kuwa refu na hata licha ya kuwataka wananchi kufuata sheria hata kwenye maeneo mengine mpaka wapewe ruhusa ya kuchimba ndipo waanze kuchimba.

Nao mshuhuda wliokuwa eneo la tukio hilo walisema kuwa marehemu Sophiani Hamisi wakati wa uhai wake alikuwa akitibu watu kwa kutumia kitabu cha dini (Quaran)na inadaiwa marahemu huyo kabla ya kuanza kuchimba dhahabu hizo alioteshwa kuwa zipo katika miamba ya eneo hilo lilopo pembeni ya nyumba  ya yake.

Kwa upande wake mjane wa mrahemu mganga wa jadi Zuena Hamisi alionyesha  kauli zenye utata alipotakiwa kuzungumzia kisa cha msiba wa mume wake uliotokana na kuchimba dhahabu kama alikuwa akifahamu harakati hizo za siku nyingi zilizokuwa zikifanywa na mumuwe kujipatia utajiri.

“Mimi sikuwepo nilikuwa kwenye msiba wa shangazi yangu huko kirumba, nimepigiwa simu kuwa mume wako amekufa akichimba dhahabu kwa hiyo mimi sijui kama kulikua na dhahabu hapo”Jambo lilowafanya wadadisi wa kisa cha mkasa huo kujiuliza kulikoni siku zote yeye asifahamu kuwepo kwa uchimbaji wa shimo hilo.

Tayari miili ya watu hao imezikwa katika maeneo tofauti ambapo mganga amezikwa katika makaburi ya waumini wa kislamu na mwili wa mfuasi wa mganga huyo ukifukiwa katika shimo walilokuwa wakidaiwa kuchimba dhahabu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.