ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 10, 2014

BancABC YAFUTURISHA MARAFIKI JIJINI DAR ES SALAAM.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum(kulia) akizungumza na wageni waalikwa wakati futari iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum(kulia) akizungumza na wageni waalikwa(hawapo pichani) wakati futari iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana.Kushoto ni Mkuu wa Huduma za kifedha wa BancABC,  Mwalimu Zubery.
Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa wakimsikiliza mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum(hayupo pichani) wakati wa futari iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana.
Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa wakichukua futari  iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana.
Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa wakila futari  iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana.
Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa wakila futari  iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana.
Na Mwandishi Wetu.
SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum amewaomba waamini wa dini ya Kiislamu kusameheana katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuwasaidia wanaohitaji msaada.

Sheikh Alhad aliyasema haya wakati wa futari iliyoandaliwa na BancABC jana katika Hotel ya Serena kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo.

"Kwa niaba ya jamii ya Waislamu ningependa kuwashukuru BancABC kwa kuandaa futari jioni ya leo ili kukumbushana katika Imani yetu ya dini ya Kiislamu. Napenda kuwaomba ndugu na jamaa wote kukaa karibu na Mwenyezi Mungu katika kipindi hiki, tukumbuke  kusameheana, kuwasaidia wale wanaohitaji msaada na kusimama imara Imani. 

Pia, naipongeza BancABC kwa kutambua mahitaji ya jamii yetu hasa wafanyakazi wa serikalini na kuamua kuanzisha bidhaa mpya ya Mkopo Rahisi iliyoenea nchi nzima. Nawatakia kila la kheri katika kutimiza majukumu yenu ya kila siku ili kuwapatia wateja wenu huduma bora zenye kiwango cha kimataifa.”, alisema Sheikh Al-haad Mussa.

Nae Mkuu wa Huduma za kifedha wa BancABC,  Mwalimu Zubery alisema, "BancABC inawathamini sana wateja wake na ni heshima sana kwetu kujumuika na ndugu zetu kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Tungependa kuwashukuru wateja wetu kwa ushirikiano wenu, hafla kama hizi zinatusaidia kuwafahamu wateja wetu vizuri ili kuweza kuwapa Huduma bora zaidi”.

Mwalim Zubery alimalizia kwa kusema, "Tungependa kuwashukuru wateja wetu wote kwa kuchagua BancABC na tunapenda kuwakumbusha wateja wetu ambao wataenda Kuhijji Macca baadaye mwaka huu watembelee matawi yetu na kupata kadi ya VISA kwa ajili ya kusafiri. 

Kadi hiyo ya VISA inahakikisha urahisi na usalama wa pesa zako uwapo popote duniani. Wateja wana fursa ya kuchagua kati ya kadi mbili za VISA za malipo ya kabla, moja ikiwa ni Cash Card na nyingine ni Travel Money Card. Kadi hizi ni salama kwa kuhifadhi fedha zako uwapo safarini nje na ndani ya nchi." 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.