ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 10, 2014

FAINALI KOMBE LA DUNIA 2014 NI ARGENTINA NA UJERUMANI

Mashabiki wa Argentina ambapo walishuhudia timu yao ikiibuka kwa ushindi wa goli 4 dhidi ya 2 za Holland, magoli yakipatikana kwa utaratibu wa mikwaju ya penati mara baada ya dakika 120 kumalizika kwa timu hizo kutoka bila kufungana. 
Mashabiki wa Argentina na Holland katika uwanja wa sao Paolo.
Argentina imejukatia tikiti ya kufuzu kwa fainali yake ya kwanza tangu mwaka wa 1990 ambapo itachuana Ujerumani.
Argentina ilikuwa imetoka sare tasa baada ya muda wa kawaida na ule wa Ziada na hivyo kulazimu mechi hiyo kuamulia kwa mikwaju ya penalti.
Kipa wa Argentina Sergio Romero ndiye aliyekuwa nyota katika mechi hiyo baada ya kuokoa mikwaju miwili na kuipa Argentina Ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Uholanzi.
Kipa wa Argentina Sergio Romero alikuwa Nyota wa mechi hiyo.
Romero aliokoa mikwaju ya Ron Vlaar na Wesley Sneijder.
Wafungaji wa Argentina walikuwa ni Lionel Messi,Ezequiel Garay Sergio Aguero na kisha Maxi Rodriguez.
Argentina sasa Itachuana na Ujerumani ambayo iliweka historia kwa kuinyuka Brazil mabao 7-1katika nusu fanali. CHANZO BBC SWAHILI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.