|
Kinana. |
KATIBU Mkuu wa CCM Taifa Abdulrhaman Kinana amewataka viongozi na waumini wa madhehebu ya dini zote kushikamana na kushirikiana katika kudumisha Amani iliyopo bila kubaguana katika misingi ya Kikristo, Kislamu na dini nyingine zilizopo hapa chini.
Kauli hiyo ameitoa juzi usiku jijini Mwanza wakati wa kujumuika katika Futari ya pamoja kwa waumini wa Kislamu na waumini wa madhehebu mbalimbali yaliyoalikwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa wa Wilaya ya Tarime Christopher Gachuma kwenye ukumbi wa Mwanza Hoteli.
“Hii ndiyo Tanzania tunayoijua, Tanzania tuliyonayo, ambayo watu wa dini zote, madhehebu yote, itikadi zote zenye tofauti mbalimbali, wanaungana wakati wote katika mema na majonzi, kudumisha umoja, amani na mshikamano miongoni mwa watanzania kama ilivyo leo hapa ukumbini.” Alisema.
Alieleza kwamba na kumuomba Mungu azikubali sara na sadaka za waumini mbalimbali wa Kiislamu na madhehebu mengine waalikwa waliohudhuria katika Futari hiyo, pia katika kuhakikisha mshikamano miongoni mwa watanzania utadumu kama Waislamu watashirikiana na Wakristo na Wahindu, watashikamana halafu sote kwa pamoja kujenga umoja na amani ya nchi yetu
Kinana alisema umoja miongoni mwa waislamu na wakristo ni jambo mhimu linalo changia umoja na ushirikiano wa watanzania bila kubaguana na kwamba, amefurahi kumuona Gachuma (ambaye alidai jina lake la Kiislamu ni Omari) akitumia uwezo aliojaliwa na Mungu kuandaa chakula hicho ambacho alialikwa kama mgeni rasmi.
“Nawaomba wale ambao Mungu amewapa uwezo mkubwa kama huu, Mweneyzi Mungu Inshaalah awakumbushe kuwasaidia wengine wasiokuwa na uwezo….. ” alisema na kwaombea wote waliofunga wamalize salama mfungo wa Ramadhani na kufika katika Ramadhani nyingine mwakani.
|
Gachuma. |
Awali Gachuma aliyepatiwa jina la Omari kutokana na utaratibu aliojiwekea wa kuwafutulisha wananchi jijini humo kwanza alimshukuru Kinana kwa kukubali wito wake na kuwa mgeni rasmi, alisema kwamba nay eye huwa Muislamu wakati wa mfungo huo lakini Kinana ni Kiongozi bora na imara anayejitahidi kujenga usawa katika Chama na nchi hivyo pamoja na sala zake, Masheikh, Mapadre, wachungaji na Maaskofu wamuombee Kinana.
|
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo. |
Akimkaribisha Katibu huyo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza mhandisi Evaristi Ndikilo alisema kwamba amani iliyopo inadumishwa kwa matendo mema kama hilo alilofanya Gachuma na kuwaomba waumini wa Kiislamu waendelee kuiombea Mwanza ili iendelee kuwa tulivu na salama ikiwa ni njia ya kudumisha mshikamano na amani.
|
Sheikh Mkuu wa Bakwata mkoa wa Mwanza, Hassan Fereji (kulia). |
Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Bakwata mkoa wa Mwanza, Hassan Fereji akitoa salamu za waislamu na Dua, aliiombea nchi iendelee kuwa na amani na kuwajalia viongozi wake wakiwemo Mkuu wa mkoa huo, Kinana na Rais Dk Jakaya Kikwete waendelee kuongoza vizuri na kuwataka wasaidizi wa Rais wamuongoze vizuri.
Sheikh Fereji alimuomba Kinana kusikiliza matatizo ya mkoa wa Mwanza na kuyafikisha kwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete ili kuyasukuma yaende kama wananchi wanavyotarajia na kuwaonya vijana nchini wazingatie maadili, wasiwatukane na kuwapiga wazee wao, Mungu hapendi, anataka wawaheshimu na kuwatii huku wakiepuka kujiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa amani.
|
Ibada ya shukuran. |
|
Wadau muhimu sana mkoani Mwanza. |
|
Mhe. Gachuma akitakiana kheri na Wazee na Viongozi wa BAKWATA. |
|
Wakati wa futuru. |
|
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula (kulia) akipata chakula pamoja na wageni wengine wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na MNEC wa Tarime Mhe. Gachuma. |
|
Akiwa na wadau wengine kwenye hafla hiyo ya futari kulia ni Diwani wa kata ya Igoma Adam Chagulani (CHADEMA) |
|
Futari mezani. |
|
Wadau wa UVCCM. |
|
Waungwana wamekusanyika hapa kufuturu pamoja. |
|
Taswira . |
|
Jiografia engo kwa engo...eneo kwa eneo. |
|
Picha ya pamoja viongozi wa meza kuu. |
|
Mkurugenzi wa Gazeti la Mzawa linalo chapishwa jijini Mwanza Mzee Nende (kulia) akiagana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana. |
|
Safu kuu. |
|
Shughuli ilimekamilika. |
.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.