ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 19, 2014

KAA TAYARI KUSHUHUDIA KIVUMBI CHA PEPSI KOMBE LA MEYA 2014.

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula (wa pili toka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kuelekea kuanza kwa Michuano ya kandanda ya Pepsi Kombe la Meya 2014 , kutoka kushoto katika picha anaonekana meneja wa Kampuni ya SBC watengenezaji wa kinyaji cha Pepsi Nicolas Coetz, Balozi wa Habari wa Pepsi Kombe la Meya 2014, na meneja mauzo wa kampuni ya Pepsi Sharif Taki. 
MASHINDANO ya Pepsi Kombe la Meya Jiji la Mwanza 2014 kuanza kutimua vumbi Agosti 2 mwaka huu na Bingwa kujinyakulia mzigo wa kitita cha Sh. Milioni sita, wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
Mwaka huu jumla ya timu 22 zitashiriki ambapo timu 12 zitatoka katika Kata 12 za  Jimbo la Nyamagana na timu nyingine 12 zitatoka katika vikundi na asasi mbalimbali za kijamii zilizopo jimboni humo.

Balozi wa Habari wa Pepsi Kombe la Meya 2014, Albert G. Sengo akizungumza na wanahabari kuhusiana na taratibu za michuano hiyo zitakavyokuwa.
Mashindano haya yanafanyika kwa mwaka wa pili mfululizo chini ya udhamini wa Kampuni ya SBC inayotengeneza vinywaji baridi kupitia kinywaji chake cha Pepsi ambapo kwa mwaka huu yameboresha zaidi kwa kuhakikisha vifaa vitakavyotolewa vinakuwa na ubora ikiwa pia na ongezeko la ukubwa wa zawadi za washindi. “Lengo kubwa la mashindano haya ni kuwezesha vikundi vya vijana wajasiriamali, kuleta umoja, hamasa, kuendeleza vipaji vya soka, mshikamano na burudani, lakini pia kuviwezesha mitaji ya kuendesha shughuli zao kupitia mashindano ya soka ili kuvijengea uwezo,” BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

Zawadi kwa washindi mwaka huu zimeongezeka ambapo bingwa atajinyakulia Bajaji ya kisasa ya kubeba mizigo na watu wanne yenye thamani ya milioni 4.5 na fedha tasilimu milioni 1.5 (jumla milioni sita), mshindi wa pili milioni 2, mshindi wa tatu milioni 1 huku mfugaji bora, timu yenye nidhamu na mwamuzi bora kuzawadiwa Sh. Laki mbili.
Awali meneja wa kamati ya mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, Bitegeko (wa kwanza kulia) alieleza kwamba timu zitakazoshiriki michuano hiyo zimegawanywa katika makundi manne ambapo kundi A litakuwa na timu sita, kundi B, C na D kila moja litakuwa na timu tano, mzunguko wa kwanza utachezwa kwa mtindo wa ligi katika makundi na hatua ya robo fainal timu zitacheza kwa mtoano hadi kupata timu mbili zitakazo cheza fainali ili kumpata bingwa kwa mwaka 2014.

“Viwanja vitakavyotumika katika michuano ya Kombe hilo ni Nyamagana, Nyegezi Kona, Mabatine Polisi, Buhongwa, Igoma Mnadani na Mkolani na waamuzi watakaochezesha mashindano hayo ni vijana wanafunzi kutoka katika Kituo cha Michezo cha Alliance cha jijini hapa,” alieleza.
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula (wa pili toka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kuelekea kuanza kwa Michuano ya kandanda ya Pepsi Kombe la Meya 2014 , kutoka kushoto katika picha anaonekana meneja wa Kampuni ya SBC watengenezaji wa kinyaji cha Pepsi Nicolas Coetz, Balozi wa Habari wa Pepsi Kombe la Meya 2014, na meneja mauzo wa kampuni ya Pepsi Sharif Taki. 
Moja kati ya kanuni za mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, zinaeleza kuwa timu itaruhusiwa kusajili wachezaji wasiozidi 25 kwa fomu zilizotolewa, Wachezaji wa Ligi kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza hawataruhusiwa katika mashindano haya.

Ni kosa kumchezesha mchezaji ambaye hajasajiliwa. Timu itakayo mchezesha mchezaji ambaye hayupo kwenye orodha ya wachezaji waliosajiliwa itapoteza michezo yote ambayo mchezaji huyo aliichezea.

Mchezaji hatoruhusiwa kusajiliwa kwenye timu zaidi ya moja. Iwapo mchezaji huyo akibainika ataondolewa kwenye mashindano na timu hiyo haitoruhusiwa kuweka mchezaji mwingine mbadala, timu itanyang'anywa pointi kwa michezo aliyo cheza mchezaji huyo.
Pepsi Kombe la Meya 2014 itafuata sheria zote 17 za soka. Kubadili wachezaji (substitution) mwisho watano. Mchezaji akipewa kadi nyekundu hatoruhusiwa kucheza mechi moja inayofuata. 

Mashindano yatasimamiwa na Kamati ya Mashindano ambayo inamamlaka ya kuifuta katika mashindano timu yoyote ambayo wachezaji wake watakuwa ni chanzo cha vurugu katika mashindano.
"Matayarisho yako safi kwa asilimia 100" says Nicolas Coetz.
*    Kila timu ina wajibu wa kutunza nidhamu ya wachezaji na washabiki wake ndani na nje ya mchezo.
*       Maamuzi ya refa yatakuwa ya mwisho katika mchezo.
*      Ni kapteni wa timu pekee ndiye anaruhusiwa kupeleka malalamiko kwa muamuzi ndani ya mchezo.
*    Timu itakayogomea mchezo itakuwa imepoteza mchezo husika na Kamati ya mashindano itakaa kuijadili timu hiyo kwa adhabu nyingine kama itaona inafaa.
*     Mchezo utaanza saa 10:30 jioni. Kila timu inatakiwa kufika uwanjani saa moja kabla ya mchezo kuanza.
*  Viongozi wa timu watatakiwa kusaini kwenye nakala ya kanuni itakayobaki kwa muandaaji wa mashindano ikiwa ni ishara ya kuwa wamezielewa na wataziwasilisha vyema kwenye timu zao ili kuboresha mchezo.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya SBC Sharif Taki alisema kwamba tangu kuanza kudhamini mashindano hayo kwa sasa yamepanua wigo na kuwa na sula ya kitaifa  na tayari yamefanyika Morogoro, Mbeya, Dodoma na wanategemea Arusha kufanyika baada ya kumalizika haya ya Jiji la Mwanza huku pia wakianda ya kukutanisha timu za bingwa kwenye Majiji ya Mwanza, Tanga, Arusha, Mbeya na Dar es salaam.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.