* Watalii toka Amerika, India, Italia na Uingereeza kufaidika na 'Airtel Tourist pack'
* Airtel yapunguza gharama za kupiga simu na intaneti kwa watalii toka Amerika, India, Italia na Uingereeza
Dar es Saalam, Juni 17, 2014, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imekuja na ubunifu mpya wa bidhaa itakayojulikana kama AIRTEL TOURIST PACK maalum kwa wageni/watalii wanaotembelea nchini toka mataifa mbalimbali ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora ya mawasiliano nafuu kwa kuwaweza kuwasiliana na ndugu na familia zao wawapo kwenye utalii wao.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema" Huduma hii mpya ya "Vifurushi vya watalii" itapunguza usumbufu kwa mtalii/mgeni kukosa mawaliano bora ya simu au Intaneti awapo katika sehemu mbalimbali ya vivutio vya utalii nchini.
Ni imani yangu kuwa wageni watafurahia huduma hii kutokana na ubora wa mawasilano ya Airtel hasa katika maeneo ya pembezoni mwa miji ambako ndiko vivutio vingi vya utalii vinakopatika.
"Kifurushi hiki cha watalii kitakuwa na muda wa maongezi wa dakika 30 za kupiga simu za nje, dakika 10 za kupiga simu za ndani ya nchi, SMS 10 kwenda mtandao wowote ndani na nje ya nchi pamoja na kifurushi cha intaneti cha 1GB vitakavyodumu kwa muda wa siku 30" alieleza Bw, Colaso
Kifurushi cha watalii Airtel Tourist Pack pia kinakuja na Laini ya simu na vocha ambapo, hii ni kwa yule mteja ambae hana laini ya Airtel au anataka kujiunga na kufaindika na huduma
Mtumiaji wa "Kifurushi cha watalii" Airtel Tourist pack atatakiwa kusajili namba yake pale tu anapofanya manunuzi kwa kutoa kitambulisho au pasi ya kusafiria. Usaliji huo utakuwa wa muda kwa siku 30 na baada ya hapo mtalii atatakiwa kutoa kopi ya kitambulisho au pasi ya kusafiria kwaajili ya usajili wa kudumu.
Huduma hii ya vifurushi kwa wageni wakutoka nje ya nchi kwa simu ni ya kwanza kutoka Airtel na inampatia mteja uhuru wa kuwasilina na ndugu jamaa na marafiki nyumbani kwa gharama nafuu zaidi kuliko ilivyokuwa awali, wateja watafurahia huduma za internet kwa kujiunga na mitandao ya kijamii, kutuma picha na video kwa gharama nafuu wakati wote . Aliongeza Colaso
Kwa upande wake mgeni rasmi, Mwenyekiti wa wadau wa Utalii nchini Bw, Gaudence Temu alisema "kwa niaba ya wadau wote wa utalii, ninaipongeza sana Airtel kwa kuanzisha huduma hii ya vifurushi vya mawasiliano kwa watalii wanaoingi nchini. Huduma hii inaendana na mahitaji ya wageni wetu na inakwenda sambamba na dhamira yetu sisi wadau ya kuendelea kutoa huduma bora katika soko.
"kwa kupitia mtandao wa Airtel ulioenea zaidi maeneo ya vijijini wageni wetu sasa watakuwa na uhakika wa mawasiliano bora na kwa gharama nafuu wakati wote" alieleza Bw, Temu
Mwenyekiti huyo pia alitoa ushauri kwa wadau wote wa biashara ya utalii kuchangamkia fulsa hiyo kwa kuwajulisha wageni wanaoingia nchini ili waweze kufaidika na punguzo hilo ambalo kwa msimu huu wa utalii hutumia gharama kubwa katika mawasiliano.
"Migahawa na Hoteli, wadau wa usafirishaji, watembezaji watalii na wadau wote hii ni fulsa kwetu kuwapa habari njema wateja wetu wanapoingia nchini kwamba kuna Tourist pak yenye faida zote hizi" alimaliza kwa kusema Bw, Temu
Vifurushi vya watalii zitapatikana katika maeneo yote ya biashara katika maeneo ya kuingia nchini kama zile viwanja vya ndege vya Dar es saalam(JKIA), Zanzibar, Arusha na KIA. Pia zinapatikana katika hoteli na migahawa ya kitalii.
Nchi zitakazofaidika na huduma hii kwa sasa ni pamoja na Amerika, India, Italia na Uingereeza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.