ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 1, 2014

TAMASHA LA SHIKOME LAADHIMISHWA KWA MWAKA WA NNE JIJINI MWANZA.

Mgeni rasmi toka Uongozi Wizara ya Habari Vijana na Michezo akihutubia kwenye Tamasha la SHIKOME linaloandaliwa na wanafunzi wa Sociology chuo cha SAUT Mwanza. Tamasha hili ambalo hufanyika kila mwaka siku ya jumamosi ya mwisho ya mwezi wa tano limelenga kuwajenga wanachuo katika Uzalendo kwa kujua mila, tamaduni na desturi za asili toka jamii na koo mbalimbali hapa nchini.  
Ngoma za jadi zimechezeka hapa.
Vyakula vyote vya asili vimelika hapa, kuanzia mahindi ya kuchemsha, viazi 'manumbu', maziwa ya mgando, supu ya ng'ombe kwani alichinjwa ng'ombe mzima kwenye tukio na vyakula vingine vingi.
Mmoja kati ya wanakamati akigawa chakula (Viazi  vitamu 'manumbu') kwa wahudhuriaji tamasha la SHIKOME Mwanza.
Ngoma za jadi.
Mapishi ya asili yakiendelea tukioni.
Moja kati ya utaratibu ambao ulikuwa ukifanywa na wazazi wetu enzi hizo katika nyakati za jioni ni kuzungumza na watoto wao, nia ma madhumuni ni kujua changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi na kwa yale makosa basi ulikuwa muda wa adhabu au maonyo. Sasa katika majira hayo ulikokwa moto kwaajili ya mwanga na kupata joto ambapo uliwakusanya wakazungumza na kutatua masuala yao mbalimbali. 
Je mwamfahamu huyu mama? 
Ngoma asili ndani ya tamasha la SHIKOME.
Huu ni uchomaji/upikaji asili wa Viazi vitamu aka 'Manumbu'  ambapo zinakusanywa pumba za mpunga na kuwekewa vipande vya moto nazo zikishika moto basi viazi vinafukiwa ndani yake vikiiva kiulaiiiini taratiiibu!! Viazi style hii vinanoga zaidi vikiliwa na maziwa mgando.
Nilikwambia Ng'ombe mzima kachinywa hapa hivyo kuna nyama choma.
Kitu 'Manumbu' na maziwa mgando. 
Mzuka ukipanda basi ngoma hupigwa kwa ngumi na siyo fimbo tena!
Eneo la tukio na jiografia yake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.