WAZIRI Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira Binilith Mahenge kuzindua
rasmi kesho maadhimisho ya kitaifa ya siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika
kitaifa jijini Mwanza Juni 5 mwaka huu mkoani Mwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana mkoani hapa, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Baraka
Konisaga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana alisema kwamba, maadhimisho hayo
yataanza rasmi jumatatu katika viwanja vya Furahisha vilivyopo Kata ya Kirumba
wilayani Ilemela ambapo yatazinduliwa na Waziri Mahenge kwa maonyesho na
shughuli mbalimbali za mazingira.
Konisaga
alieleza kuwa kutokana na heshima ya kupewa hadhi kwa mkoa wa Mwanza ya kuandaa
maadhimisho hayo ya kitaifa ya kila mwaka, kumeandaliwa shughuli mbalimbali
ikiwemo maonyesho kutoka kwa wadau mbalimbali wa mazingira ndani na nje ya
nchi, vikundi na wananchi kushiriki katika kufanya usafi katika maeneo ya Jiji
na Manispaa ya Ilemela ikiwa ni sehemu ya Jiji la Mwanza.
“Maadhimisho
ya mwaka huu yanayo kauli mbiu ‘Tunza Mazingira Ili Kukabiliana na
Mabadiliko ya Tabianchi’ lakini pamoja na maonyesho hayo zitakazofanyika
ziara katika maeneo tofauti yanayojihusisha na utunzaji wa mazingira ikiwemo
viwanda jijini hapa, pia shughuli za uopoaji magugu maji ndani ya Ziwa
Victoria, upandaji miti, uzoaji taka na kuhamasisha wananchi na wadau kwa
makongamano,” alisema.
Aidha
Kaimu huyo aliongeza kuwa ya uzinduzi huo, Kamati ya kitaifa ya Maadhimisho ya
kilele cha siku ya Mazingira Duniani itaendelea na utaratibu wa kuandaa
taratibu za utoaji Tuzo, Zawadi na Veti kwa washindi na wadau mbalimbali mambo
mengine huku Juni 5 mwaka huu itakuwa
ndiyo kilele chake ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilali.
“Tutakuwa
na ugeni mkubwa wa kitaifa na kutakuwa na wageni wengine kutoka sehemu
mbalimbali ya nchini ambao ni wadau wa
mazingira na kutoka mataifa ya nje, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na mashirika
ya kimataifa yanayojihusisha na mazingira” alisisitiza.
Ametoa
wito kwa wananchi kuendelea na jukumu la usafi na kuliweka Jiji la Mwanza na
Manispaa ya Ilemela katika mwonekano halisi wa kupokea tuzo na wageni hao ili
kuwezesha pia kutangaza vivutio mbalimbali vya uwekezaji, utalii na maliasili
ya Jiji hili linalikuwa kwa kasi ya asilimia 11 kila mwaka barani Afrika huku
pia akiwataka kujitokeza kwa wingi katika maonyesho na siku ya kilele cha
maadhimisho hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.