ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 2, 2014

NITAPELEKA USHAHIDI ROMA KUHUSU MAISHA YA NYERERE - MUSEVENI

Picha ya mwisho ya Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere aliyopigwa kijijini kwake BUTIAMA kabla ya kwenda kupata matibabu nchini Uingereza ambapo alifia katika Hospitali ya Mt. Thomas. 
SIKILIZA MAHOJIANO YANGU NA Mmisionari Simon Nyirani Mhagama wa Shirika la Mt. Kalorilwanga

KUTOKA Uganda:Rais Museveni alisema natarajia kupeleka ushahidi kwa Papa Benedict kwamba Mwalimu anasifa za kutangazwa kuwa mtakatifu kwa sababu alimtii Mungu na kuwatumikia binadamu. "Mimi nitapeleka ushahidi kwa Papa, kwamba mbali na mwalimu kumtii Mungu na kuwapenda binadamu wote, pia aliwakomboa Waafrika kutoka Ruvuma mpaka Capetown, huu ni ukweli siyo hadithi, alisisitiza Rais Museveni.


Rais Museveni aliyasema hayo (Junimosi) wakati wa ibada ya kuombea mchakato wa kumfanya Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa mwenyeheri na hatimaye kutangazwa mtakatifu.

Kufuatia hatua hiyo ya kwenda Roma kutoa ushahidi, Rais Museveni amesema katika maadhimisho ya kuombea mchakato wa Mwalimu kuwa Mtakatifu yatakayofanyika mwakani, ameahidi kuwaita maraisi wote waliowahi kufanyakazi na Mwalimu Nyerere ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa Marehemu Baba wa Taifa ameweza kuwa unganisha Waafrika.

Alifafanua kuwa Mwalimu ametoa mchango mkubwa wa ukombozi kwa nchi za Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Namibia, Angola, Afrika Kusini, Uganda na Tanzania yenyewe. Hivyo kuja kwa viongozi hao kushiriki ibada hii itakuwa Baraka kubwa.

Rais Museveni ambaye alitumia muda mwingi wa hotuba yake kuzungumza Kiswahili, alisema baada ya jitihada za mwalimu kuikomboa Uganda, ndipo nawao walipoweza kuzisaidia nchi za Rwanda, Sudan Kusinina Congo kujikomboa na kuongeza kuwakama sijuhudi za mwalimu wasingekuwa na uwezo wa kuwasaidia wengine.

Rais Yoweri Museveni, amesema kiongozi bora ni yule anaye fuata maagizo ya Mungu na kuwatumikia binadamu wote kwa usawa na haki."Kwenye biblia kuna sehemu inauliza kuwa utampendaje Mungu ambaye hujawahi kumuona, na ushindwe kumpenda binadamu mwenzako," Alisema kwa sababu aliwahi kufanyakazi na mwalimu, anaweza kutoa ushahidi kwamba mwalimu alifanya yote mawili, kumtii Mungu na kuwatumikia binadamu.

Alisema mojawapo ya sababu iliyomfanya Marehemu Papa Paulo IIkutangazwa mtakatifu kuisaidia Ulaya Mashariki, ambayo wananchi wake walikuwa hawamwamini Mungu.
"Marehemu Papa Paulo IIalisaidia kuikomboa Ulaya Mashariki kutoka kwenye ukomunisti, wananchi walikuwa hawaamini kama kuna mungu, lakini kwa juhudi zake aliwafanya wamwamini na kumpenda Mungu,"alisema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.