|
Catherine Palmer (20) |
|
Patricia Phinias (22). |
|
Connie Frederick (21) |
|
Asia Mohamed (20) |
|
Coletha Jastine (21) |
|
Esthar Martin (22) |
|
Caroline Akut (21) |
|
Mariam Yusuph (19) |
|
Reira Abeid (21) |
|
Elizabeth Gordian (21) |
|
Huyu ndiye Matron wa washiriki wa Redds Miss Simiyu 2014 Bi. Clara Ayoub. |
|
Washiriki katika picha ya pamoja. |
|
Sehemu ya waalikwa na waandishi wa habari walio hudhuria tukio la utambulisho wa wanyange hao ambao watakwenda kushindanishwa katika kinyang'anyiro hicho kitakachofanyika mnamo tarehe 7/06/2014 mkoani Simiyu. |
|
Mratibu wa Redds Miss Simiyu 2014 omary Bakari (katikati) akiwa na wanyange wa kinyanganyiro kitakacho fanyika tarehe 7/06/2014 mkoa mpya wa Simiyu. |
WAREMBO 16 kutoka Wilaya tano za Mkoa wa Simiyu wameingia kambini kujiandaa na kinyang’anyiro cha kuwania taji la REDD'S Miss Simiyu lililopanwa kufanyika Juni 7 mwaka huu mkoani hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Muandaaji wa shindano hilo Mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2014/2015, Omary Bakari, alisema kwamba tayari warembo 16 wako kambini kuanzia juzi watakaoshiriki shindano la REDD'S Miss Simiyu kutoka Wilaya za Bariadi, Busega, Itilima, Maswa na Meatu.
Bakari alisema kwamba shindano hii ni mara ya kwanza kwa Mkoa wa Simiyu kuaandaa na kushiriki mashindano ya kumsaka warimbwende watakao uwakilisha Mkoa huo katika shindano la Kitaifa la REDD'S Miss Tanzania mwaka 2014/2015 baada ya Wilaya zake kugawanywa na kuundwa Mkoa mpya wa Simiyu.
“Tayari wadhamini wa shindano hili wameisha kamilisha taratibu za udhamini wao kwa kufunga mkataba ambao umewezesha warembo hawa 16 kuingia kambini kujifua kwa kuanza mazoezi, kufundwa kimaadili na kuonyesha vipaji vyao na matarajio yao katika kuisaidia jamii endapo watafanikiwa kuwa washindi chini ya mkufunzi wao Clara Ayoub ” alisema.
Mratibu wa shindano hilo, alisema kwamba katika kunogesha shindano hilo siku hiyo kwa mara ya kwanza wananchi wa Mkoa huo watashuhudia burudani kali kutoka kwa mwanzamuziki mashuhuri wa Muziki wa Taarabu nchini Mzee Yusufu na kundi zima la Jahazi Modern Taarab, Msanii wa Bongo Fleva H Baba na wasanii wengi kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo wachekeshaji.
“Wito wangu kwa wananchi wa Mkoa wetu wa Simiyu wajitokeze kwa wingi kujionea vipaji vya warembo ambao wana sifa zote zinazokidhi vigezo vyakuwa washindi na kutoa Baraka zao kwa warembo wawili watakaouwakirisha mkoa huu katika shindano la kitaifa mwaka huu” alisema.
Bakari aliwataja wadhamini wa REDD'S Miss Simiyu mwaka huu kuwa ni Kampuni ya Airtel, TBL kupitia kinywaji chake cha REDDs, Chuo cha Musoma Utalii Mkoa wa Shinyanga, Bhatt Electronic, Serengeti Stop Over, Benki ya CRDB, SBC kupitia kinywaji cha Peps, G&K Smart Hotel, Victoria Insitute, Matvila Beach na LP Gass Point.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.