TASNIA ya muziki wa dansi nchini Tnzania imepata pigo mara baada ya mmoja kati ya mwimbaji nyota wake aliyewahi kufanya vyema Amina Ngaluma 'Japanese' kufariki dunia.
Muimbaji huyo aliyetamba na bendi za Tam Tam na Double M Sound, amefariki dunia jana akiwa nchini Thailand alipokuwa akiishi kikazi.
Kwa mujibu wa mume wa marehemu ambaye pia ni mwanamuziki Rashid Sumuni, amethibitisha kifo cha mkewe na kuongeza kuwa mkewe alikuwa nchini humo akiwa na mkataba wa moja ya bendi nchini Thailand inayojulikana kwa jina la Jambo Survival aliyokuwa akiimba.
Siku nne zilizopita alipata taarifa kutoka kwa kiongozi wa bendi hiyo Hassan Shuu kuwa marehemu mkewe amekimbizwa hospitali mara baada ya kupata maumivu makali ya kichwa.
Mpaka anakimbizwa kupatiwa matibabu kwenye moja ya hospitali kubwa nchini Thailand inatajwa kuwa alikuwa katika hali mbaya kiasi kwamba ilifika kipindi marehemu 'Japanese' alizidiwa hata akawa hajitambui.
"Toka jumamosi alikuwa hajitambui na jana majira ya saa 6 nilipata simu kuwa mke wangu kaaga dunia" Alisema Rashid Sumuni wakati akihojiwa na Amplifaya ya Clouds fm.
Moja ya nyimbo zilizompa umaarufu ni Mgumba No.1 aliouimba na bendi ya African Revolution 'Tam Tam' chini ya Mwinjuma Muumini.
G. Sengo blog inapenda kuwapa pole ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa familia, mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.