ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 15, 2014

MKUU WA MKOA WA MWANZA INJINIA NDIKILO AFUNGUAA MKUTANO WA 16 WA WAKANDARASI NA WADAU WA UJENZI

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano wa Bodi ya Usajiri wa Makandarasi kwa mwaka 2014 kwa Kanda ya ziwa uliofanyika katika kituo cha mafunzo Benki Kuu Capri Point Mwanza.
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Eng. Boniface Muhegi amesemakuwa idadi ya makandarasi daraja la Kwanza imeongezeka toka 15 kwawalioomba kupandishwa daraja hadi kufikia 40.
Unapozungumzia ujenzi wa miundombinu kama barabara, reli, bandari, viwanja vya ndege, viwanda, mabwawa na malambo ya maji, migodi ya madini, makazi ya watu, majumba ya starehe, hospitali, shule na minara ya mawasiliano, moja kwa moja unawagusa makandarasi. Sasa wamekusanyika hapa kuhudhuria Mkutano wa 16 wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa makandarasi kwa mwaka 2014 kwa Kanda ya Ziwa uliofanyika katika kituo cha mafunzo Benki kuu Capri Point Mwanza.
Bodi ya Makandarasi imekuwa ikitumia mikutano hii kupata mrejesho kutoka kwa wadau pamoja na kutathimini maeneleo ya sekta ikiwani pamoja na kuibua mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili na hivyo kuleta maendeleo kwa Makandarasi, husussani Makandarasi wazalendo.
Ili kuinua uwezo wa Makandarasi Bodi ya makandarasi imekuwa ikiendesha mafunzo mbalimbali chini ya Mpango Endelevu wa Makandarasi unaopewa sapoti na Mfuko wa kusaidia Makandarasi (Contractors Assistance Fund), pamoja na Mkakati Maalum chini ya Mpango Maalum wa Kuendeleza Makandarasi wa Kizalendo. 
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Eng. Boniface Muhegi " Sheria ya kulipa kodi ya mwaka ilibadilika miaka mitatu iliyopita Makandarasi waliosajiliwa miaka mingi iliyopita walikuwa wamekariri kuwa zamani ulikuwa unaweza kulaza miaka miwili bila kulipa na usifutwe, lakini kwa sasa sheria hairuhusu kulaza mwaka wowote, na usipolipa sheria mama inakutaka usiendelee kuwa Mkandarasi. Sasa hii imekumba makandarasi wengi sana.. CRB imefuta Makandarasi 752 tulisikitika sana, lakini kwasababu ilikuwa ni kwa mujibu wa sherika hatukuwa na lakufanya"
Wakandarasi wameombwa kuweka wataalamu katika kusimamia shughuli zao za utendaji na kufanya kazi kwa viwango bora ili kupata thamani halisi ya fedha na kuendelea kuwa na sifa.
Kusanyiko la Makandarasi ndani ya ukumbi wa BOT Capri point Mwanza.
Makandarasi kutoka mikoa ya Mwanza, Simiyu, Kagera, Mara, Geita, Shinyanga na Tabora wakifuatilia ufunguzi wa  Mkutano huo kwa umakini. 



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.