Kuona hali hiyo ndipo wadau hao wa burudani walipo wekeana dau la pesa na kisha kununua mayai yote aliyokuwa nayo kiasi cha trey moja na nusu na kumkabidhi kijana huyo kisha akaanza kula mbele yao ambapo kadri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo imani ya kuamini juu ya uwezo wa kijana huyo ilivyokuwa ikiwaingia huku wengine wakibisha kwa maneno "Ah wapi atatepeta tu huyo subirini, hawezi kumaliza mayai yote haya". Mmmmh kumbe walikosea!!
Issa Mataarabu aliendelea kula moja baada ya jingine hatimaye ngoma ikabaki mayai nusu trey huku wala asihitaji chumvi wala maji...loh salaleee!!!
Wengi waliojumuika kwenye eneo la tukio walikuwa na hasira kutokana na maswali yao mengi kukosa majibu kwamba inawezekanaje kijana mdogo kama huyo aliye na umbo dogo tu bila kuonyesha dalili ya kitambi anawezaje kula kiasi kikubwa hicho cha mayai bila kushiba?
Huku wengine wakidai kuwa kijana huyu yawezekana katumwa kwa njia ya kimazingira na watu au mizimu kuishibisha Athumani Mataarabu yeye aliendelea kula na kula na kula huku mmoja kati ya wanamishezo washiriki wa Bonanza la Maveterani (juu kwenye picha) akimsaidia kumenya mayai hayo ili kijana huyo awe na kazi moja tu .....kula.
Mayai aliyamaliza na kwa hasira wadau hao waliokuwa wakibishana wakaaamua kumtimua. Hakuishia hapo alihamia kwa wadau wengine na kukutana na mzigo kama ule ule ambao nao aliutendea haki...Duh! SIKILIZA WADAU WAKIZOZANA:-
Issa Mataarabu ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watatu, kati ya wote hao ndani ya familia yao ni yeye tu mlaji wa kupitiliza wengine wanakula kawaida tu.
Kwa mujibu wa mama Sauda Chiza, mama anayeishi naye jirani alikiri kumtambua Issa pamoja na uwezo wake, akisema kuwa ndugu zake wamemtenga hawataki kuishi naye kwani hawawezi kumudu bajeti yake na hata ikitokea harusi mtaani kwao kijana huyo hufika jikoni kuomba hisani ya akinamama wampe chakula kilichobaki au hata ukoko kwani hajashiba, na kwasababu wanamfahamu basi umhurumia na kumpa kilichopo sambamba na ukoko wa masufuria yote yaliyopo. MSIKILIZE JIRANI ANAYEISHI NAYE MTAA MMOJA:-
Dubwi...dubwiii!!! Kama anatumbukiza vile kwenye mfuko na si tumboni. |
Anaongeza kuwa siku ambayo alikula chakula kingi mpaka akashiba ile barabara ni siku alipokula mlo wa mchana ugali unga kilo 6, maharagwe kilo moja na nyama kilo moja.
Issa ambaye wazazi wake walitengana hivi sasa anaishi kwenye chumba cha kupanga huko Kirumba biashara ya mayai ndiyo inayoendesha maisha yake, akiwa ni mwajiriwa (mchuuza mayai ya kuchemsha) huuza mayai ya kuchemsha ya mdau mmoja anayeishi karibu na alikopanga kwa makubaliano ya malipo ya shilingi 1,000/= kwa kila trey, ambapo anauwezo wa kuuza trey 4 kwa siku.
Ana uwezo wa kula chapati 30 na chai themosi mbili za vikombe 12 kama kifungua kinywa, mchana ugali kilo 2 na usiku kilo 2.
Anawezaje kujikimu ile hali kipato na uchumi ni duni; MSIKILIZE ISSA MWENYEWE AKIZUNGUMZA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.