ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 21, 2014

KITU FRESH TOKA ZIWA VICTORIA

Mpishi akikatakata samaki aina ya Hongwe kupata vipande vya kupika, nako sufuriani kuna samakia aina ya sato ambao tayari wamesha pitia sevisi' zote ikiwa ni pamoja na kuparuriwa magamba, kutumbuliwa na mengineyo muhimu kwa ajili ya either kukaangwa au kuchemshwa.
Seksheni ya ukataji kwa ukaribu.
Live bila chenga.
Akicharangwa kupata vipande.
Vipande.
KAMA ulikuwa haujui Sangara ni samaki mvamizi. Si samaki asili katika ziwa Victoria.Samaki huyu ameleta faida kubwa kwa upande wa 'Pato la Taifa' pamoja na kuzalisha wafanyabiashara wakubwa viongozi na matajiri wa nchi  hii. 

Samaki wa asili (Endermic Species) wa ziwa Victoria ni Sato, Nembe, Gogogo, Ningu, Soga, Dagaa, Furu, Kamongo, Ngege, Mumi, Hongwe, Mbofu, Kuyu... (dah wegine nitaongeza hapa hapa nikikumbushwa).

Lakini yote kwa yote samaki hawa wanaopendwa kote ambapo kutwa licha ya kutumiwa kama kitoweo na wenyeji pia wamekuwa wakiagizwa kwa mafungu makubwa, tani na tani na waishio mbali, samaki hawa ni watamu na wenge lishe bora hasa pale wanapoliwa fesh (kitu mchemsho).
Kaaazi kweli kweli. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.