Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Stephen Kebwe (kulia). |
Matokeo ya tathimini hiyo yameonyesha kuwa wakati mikoa ya Kanda nyingine nchini imekuwa na maendeleo ya kuridhisha katika ongezeko matumizi ya huduma za uzazi wa mpango mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo mkoa wa Mwanza na ile ya kanda ya Magharibi inaendelea kuwa na kiwango kidogo zaidi cha utumiaji wa huduma hiyo.
Mkoa wa Kilimanjaro umeongoza kwa utumiaji wa huduma za uzazi wa mpango ambapo watu wake wamekwea asilimia 50 kwa matumizi ya huduma hiyo, ikilinganishwa na mkoa wa Mwanza wenye matumizi kidogo ya asilimia 12 tu.
Katika uzinduzi huo igizo la kuelimisha masuala ya uzazi wa mpango lilifanyika katika viwanja vya Nyamagana. |
Somo limekolea, maswali na majibu ndani ya igizo hadi mwisho wa siku somo likaeleweka. |
Baadhi ya Wadau wawezeshaji wa Uzazi wa Mpango wakifuatilia matukio yanayoendelea kwa umakiiiini! |
Akina mama wananchi wa Mwanza. |
Katika viwanja hivi huduma ya uelimishaji imefanyika na hapa ni wadau wa UMATI wakitoa elimu kwa wananchi mbalimbali waliodhiru banda lao. |
Mpango wa afya. |
Uwiano kati ya uzito wa mwili na urefu unasababu katika afya kamili ya kila mmoja wetu. |
BMI hupatikana kwa kugawanya Uzito (Weight in Kg) kwa (Kimo mara Kimo) (Kimo/Height in M) au Uzito (Weight in Kg) gawanya kwa (Kimo mara Kimo) (Kimo/Height in Cm). Jibu utakalopata, zidisha kwa 10,000 au Uzito (Weight in Lb) gawanya kwa (Kimo Mara Kimo) (Kimo/Height in In) na Jibu utakalopata zidisha kwa 703.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.