Maadhimisho hayo yanataraji kufanyika Juni 5 mwaka huu, chini ya uratibu wa Wizara ya Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu kabla ya zawadi
na Tuzo hizo kutolewa na ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.
Hida aliwataka wataalamu na watendaji wa Jiji hilo kujiandaa
na maadhimisho hayo, ambapo tayari ofisi ya Waziri Mkuu imeisha toa vigezo vya
kushindaniwa na Majiji, Manispaa na Halmashauri za wilaya nchini kote.
“ Watendaji wa Kata na Mitaa tuendelee na mkakati
wetu wa usafi kwenye Kata na Mitaa ikiwa ni pamoja na kuendelea kuweka
mazingira yetu katika hali ya usafi ili jiji hilo liibuke tena na tuzo ya
ushindi kwa mara ya tisa mfululizo,” alisisitiza
Mkurugenzi Hida alisema juzi kwamba, “Tutumie sheria
ndogo ndogo za Hamashauri yetu na kuhamasisha wananchi na vikundi vya usafi
kuweka mazingira katika hali ya usafi kabla ya wakaguzi kupita kwenye Mitaa na
Kata kutoa maksi.” Alieleza.
Aidha alifafanua kwamba, pia katika maadhimisho hayo
jiji linategemewa kupata wageni kutoka Majiji, Miji, Manispaa na Halmashauri za
Wilaya za ndani na nje ya nchi, ambao wamekaribishwa
kushiriki katika maadhimisho hayo.
Huku akitamba kunyakua ushindi kwa mara ya tisa,
Hida aliwaagiza maafisa afya wa jiji hilo kuweka mikakati ya kuendeleza usafi
katika jiji hilo aliloliita Smart City ili kuwa kivutio kwa wawekaezaji na
wageni watakaokuja.
Kwa upande wake, Meya wa Jiji hilo Stanslaus Mabula
amemtaka Mbunge wa jimbo la Nyamagana Ezekia Wenje aache kuwachochea
wafanyabiashara ndogondogo (machinga) na kuwachonganisha na viongozi wa serikali
na Jiji ili wavunje taratibu, kanuni na sheria za Mipango miji.
Meya, Mabula akihutubia Baraza la Madiwani wa jiji
hilo, alisema kwamba licha ya Wenje kutoshiriki mara kwa mara vikao vya baraza
hilo, lakini amekuwa akiwahamasisha wamachinga
na wafanyabiashara wengine kufanya biashara katika maeneo wasiyo ruhusiwa
jambo ambalo linaweza kusabaisha jiji hilo lipoteze ushindi.
“Kwa hili niwaombe wafanyabishara wanaofanya
biashara katika maeneo yasiyo ruhusiwa ikiwa pamoja na wanaopanga bidhaa nje ya
maduka na sehemu za wapiti kwa miguu, waache mara moja kwani wanavunja sheria
ya mazingira ya mwaka 2004 kifungu namba 187 (1) na 191 Act Cap 20/2004.”
Alisema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.