Nje ya Ukumbi maarufu wa Mikutano na Harusi wa Royal Sunset Beach Resort uliopo Luchelele Mkolani Wilayani Nyamagana. |
Vingozi wakiwasilindani ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mwanza leo. |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo mjumbe (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dkt. Anthon Dialo wakiwasili ndani ya ukumbi tayari kuanza kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa. |
Wakuu wa Wilaya walialikwa kushoto ni Mariam Rugaira (Misungwi), Mary Tesha (Ukerewe) na Seleman Mzee (Kwimba) wakionyesha furaha ndani ya kikao. |
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dkt. Dialo akiongoza duah ya kuwaombea wajumbe wa kikao hicho waliotangulia mbele ya haki. |
Ni wakati wa dakika moja ya kuwakumbuka wenzetu kwa duah kabla ya kuanza kikao hiki. |
Meza Kuu, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Joyce Masunga "Maziwa Fresh" akitoa neno kabla ya ya kumkaribisha mwenyekiti wa CCM Mkoa Dkt.Dialo kufungua kikao. |
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dkt. Dialo akiongoza kikao. |
Hapa mbele ni Sekretarieti ya CCM Mkoa wa Mwanza ikiwajibika. |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo mjumbe akitoa maelekezo ndani ya kutano. |
Na Peter Fabian.
MWANZA.
PATO la wakazi wa Mkoa wa Mwanza limeongezeka kutoka shilingi 829,447 kwa mwaka 2010 hadi kufikia shilingi 910,824 mwaka jana kutokana na utekelezaji mzuri wa mipango na Ilani ya uchaguzi ya CCM Mkoani hapa.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo wakati akiwasilisha taarifa ya serikali ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mwanza katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Royal Sansert Luchelele Kata ya Mkolani Jijini hapa.
Injinia Ndikilo alisema kuwa, serikali ya CCM imechapa kazi na inastahili pongezi kwani mkoani mwake, kipato kimeongezeka kwa mwananchi mmoja mmoja ambapo sasa kimefikia laki 9.8 kwa mwaka jambo ambalo imelitekeleza kwa vitendo kwa kuwaonyesha wananchi fursa sanjari na miradi yote ya maendeleo na kiuchumi inayotoa huduma kwa jamii kwenye maeneo mbalimbali ya Wilaya za Mkoa huo.
Taarifa hiyo imeonyesha kuongezeka kwa kasi ya kusambaza umeme vijijini ambapo zaidi ya vijiji 210 katika Wilaya saba (7) vinapatiwa umeme na miradi ya maji ipatayo 138 inajengwa katika wilaya za Magu (13), Sengerema (13), Kwimba (58), Ukerewe (13), Misungwi (31) na jijini Mwanza ni kumi.
“Katika maelekezo ya Ilani yanaelekeza kukamilisha upelekaji umeme kwenye mikoa na wilaya ambazo hazijafikiwa na kupitiwa na Gridi ya taifa. Tayari serikali imeandaa mkakati kabambe wa kupeleka umeme vijijini kupitia mradi wa usambazaji ujulikanao kama ‘Electricity V’ ambao sasa umeanza kutekelezwa kwa kumshirikisha Wakala wa Nishati Vijijini (REA).” Alieleza.
Mkuu huyo, Alisema kuwa mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa mkoa wa Mwanza uko katika wilaya za Kwimba, Sengerema, Misungwi na Magu ambapo zitajengwa njia za umeme wa msongo wa kilovolti 33 wenye jumla ya kilometa 290 na kusambaza vijiji zaidi ya 40.
Aidha mradi mwingine ulio chini ya REA awamu ya pili ambao uko kwenye wilaya zote za mkoa huo zikiwemo za Ilemela, Nyamagana na Ukerewe ambao utasambaza nishati hiyo katika vijiji vingi zaidi ya 171 na kufanya miradi hiyo ifikie vijiji zaidi ya 210.
“Kumekuwepo na baadhi ya wanasiasa wanaotamba kwenye majukwa ya kisiasa na kusema serikali ya CCM haiwezi kuwaletea maendeleo wananchi ni hao ni waongo na wanaowapotosha wananchi. Kwenye sekta ya maji upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama umeongezeka na kufikia imefikia aslimia 56 mwaka 2013 na mijiji asilimia 74 ambapo hadi kufikia 2015 vijijini itakuwa asilimia 65 na mjini asilimia 75.” Alisema.
Alifafanua kwamba katika vijiji vya Wilaya za Ukerewe ni asilimia 62, Ilemela 51, magu 63, Sengerema 59, Misungwi 40, Kwimba 46 na Nyamagana 51 huku katika miji ya Nansio ikiwa asilimia 30, Ilemela 90, Magu 17 Sengerema 42, Misungwi 41, Ngudu 46 na Nyamagana 90.
Baada ya taarifa hiyo kupokelewa na kupongezwa baadhi ya wajumbe walihoji utekelezaji wa taarifa hiyo na wengine wakitaka serikali kuongeza kasi ya utekelezaji wa sekta za maliasili na utalii, afya, uvuvi, kilimo, miundombinu ya barabara, elimu na ardhi na uwekezaji ikiwemo pia usafi na mazingira.
Mjumbe Bitulo Kazeli aliwataka viongozi na watendaji wa serikali kuu na Halmashauri zote za Mkoa huo kuweka mkakati maalumu na kuzingatia utekelezaji wake katika sekta ya kilimo ambayo asilimia 75 ya wananchi ni wakulima kwa kuanza kutekeleza kilimo cha umwagiliaji katika maeneo mbalimbali ili kuwa na uhakika wa chakula ambapo kasi yake imeonekana kuwa ya kusuasua.
Awali Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza Anton Diallo akifungua kikao hicho alisema kwamba hakuna utaratibu mzuri kwenye baadhi ya Wilaya wa fedha za Chama kufika kwenye Kata na Matawi kutokana na baadhi ya viongozi wamekuwa hatekelezi maagizo yanayotoka ngazi za juu na hivyo wamekuwa wakigawana posho za bure bila kutimiza wajibu wao.
“Hili tunaendelea kulifanyia kazi na tunaendelea kuwasisitiza viongozi kufikisha fedha hizo kwenye maeneo yaliyolengwa pamoja na kuhakikisha wanafanya vikao vya ngazi husika kwa kufuata kalenda ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo ya mkutano mkuu wa Chama uliofanyika Dodoma mwaka jana na kukutana na wanachama na kusikiliza kero za wananchi na kuzifanyia kazi” alisisitiza.
Kikao hicho maalumu cha Halmashauri kuu ya CCM Mkoa kilimjumuisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Kamanda wa Polisi Mkoa, Wakuu wa Wilaya zote saba (7) za Mkoani humo, Meya wa Jiji la Mwanza, Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri za Wilaya zote, wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa na wanachama na Makada wa chama hicho.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.