ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 22, 2014

MUUMINI AMLILIA GURUMO, DOUBLE M SOUND YAFUFUKA.

Muumini akiwa kwenye mahojiano na mtangazaji wa Radio Kwizera Seif Omary Upupu. 
Mkurugenzi wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya Double M Sound Mwinjuma Muumini amesema ameumizwa sana na kifo cha Gwiji wa Muziki wa Dansi Nchini Muhidin Maalim Gurumo kwa kuwa kimesababisha asifikie baadhi ya malengo yake Kimuziki.
Amesema kilichomsikitisha zaidi ni kuona Mzee Gurumo amefariki kabla hawajatimiza malengo ya kufanya kazi za pamoja kutokana na kukabiliwa na maradhi mfululizo. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Kocha wa dunia Mwijuma Muamini akiwa amevua nguo na kubaki na bukta baada ya wazimu kumpada wakati akiimba wimbo wa Fadhila kwa Wazazi part 2 (hapa ni katika kile kibwagizo wazimu wangu ukinipanda hata nguo nitavua......) 
Katika mahojiano na mwenzangu Seif Omary Upupu wilayani Ngara Mkoani Kagera alikokuwa amekekwenda kufanya Tamasha la Jumatatu ya Pasaka, Mwinjuma amesema Mzee Gurumo alikuwa akiwasaidia wanamuziki wengi katika ushauri wa masuala mbalimbali ya Kimuziki.
Pia amewaomba Watanzania kumpigia kura katika Tuzo za mwaka za Kilimanjaro Music Award’s kwa kuchagua wimbo wake wa SHAMBA LA BIBI kuwa wimbo bora wa Kiswahili kwa kuandika (SMS AC2 kisha tuma namba 15440).
Ally Akida na gitaa lake.
Muumini Mwinjuma amefanya Onesho mjini Ngara Mkoani Kagera katika Ukumbi wa New Happy akiwa na Band yake ya Double M Sound aliyoianzisha upya ambapo miongoni mwa nyimbo zilizoonekana kugusa hisia za mashabiki wake wengi ni Wimbo wa Shamba la Bibi, Kilio cha Yatima, Fadhila kwa Wazazi-II
Muumini akiwa na Seif Omary Upupuu mara baada ya kutembelea kituo hicho.
Baada ya miaka kadhaa ya ukimya wa Bendi yake ya Double M Sound aliyodai ilikufa kifo cha kawaida kutokana na uchakavu wa vifaa, Muumini amelazimika kukimbia jijini Dar Es Salaam na kuweka maskani mjini Kahama mkoani Shinyanga ambako ameifufua Bendi hiyo na kuahidi makubwa zaidi katika Bendi yake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.