ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 22, 2014

UZINDUZI WA KAMPENI YA KUTOKOMEZA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KWA MAMA MJAMZITO AU ANAYENYONYESHA KWENDA KWA MTOTO KUFANYIKA TAREHE 29APRIL 2014 MWANZA.

Afisa Uhusiano wa Tume ya Kikriso ya Huduma za Jamii (CSSC) Renatus Sona (katikati) akiwasilisha taarifa ya Uzinduzi wa kampeni maalum ya kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito au anayoenyonyesha kwenda kwa mtoto (OPTION B PLUS) itakayoanza rasmi tarehe 29 April 2014 katika Hospitali ya Sekoutoure jijini Mwanza.
Afisa Uhusiano wa Tume ya Kikriso ya Huduma za Jamii (CSSC) Renatus Sona
CSSC kwa kushirikiana na RHMT chini ya uongozi wa mganga mkuu wa mkoa inatarajia kufanya uzinduzi rasmi wa Option B Plus mkoani Mwanza tarehe 29/04/2014. Malengo makuu ya uzinduzi huo ni;
1.Kuhamasisha na kuongeza uelewa kuhusu OPTION B PLUS katika jamii.
2.Kutambua mchango wa watoa huduma wa afya na kuinua ari katika kutekeleza mpango huu.

Uzinduzi huo utatanguliwa na maandamano yatakayoanzia katikati ya mji hadi viwanja vya Hospitali ya mkoa Sekou Toure, utoaji wa huduma ya  mama na mtoto, shuhuda kutoka kwa wamama wajawazito wanaoishi na VVU, hotuba ya mgeni rasmi, risala kutoka kwa wadau mbalimbali wanaotoa huduma ya kupambana naUKIMWI pamoja na ujumbe wa Option B plus kupitia vikundi vya ngoma vya uelimishaji.
Mmoja kati  ya madaktari wasimamizi wa kampeni hiyo akizungumza na waandishi wa habari jinsi kitengo chake kilivyojipanga kuhakikisha mpango huo unaleta matokeo chanya kwa jamii.
Waandishi wa habari wakisikiliza utaratibu na matayarisho ya Uzinduzi wa kampeni maalum ya kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito au anayenyonyesha kwenda kwa mtoto (OPTION B PLUS) itakayoanza rasmi tarehe 29 April 2014 katika Hospitali ya Sekoutoure jijini Mwanza.
Daktari wa watoto wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Dr. Shinje Peter Msuka 
CSSC kwa kushirikiana na Wizara ya Afya inatekeleza mradi huu kwa kutoa huduma za upimaji wamama wajawazito, wanaonyonyesha na watoto waliozaliwa na mama wanaoishi na VVU, utoaji dawa na kutoa elimu kwa jamii ya ushirikishwaji wa wanaume katika suala zima la kuzuia maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Afisa wa PMTCT DR. Benedict Andrea. 
Kwa kutekeleza jukumu hilo CSSC kwa kushirikiana na Wizara ya Afya inaendelea kutoa mafunzo kwa kutoa huduma ya Afya katika vituo vya kutolea huduma vya mkoa wa Mwanza, ambapo mpaka sasa watoa huduma wapatao 557 wa kutoka vituo 222 wameshapewa mafunzo ya kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Hii ni sawa na asilimia 87.4 ya idadi ya vituo vya Afya na watoa huduma waliotakiwa kupewa mafunzo hayo kwa mujibu wa muongozo wa Wizara ya Afya.

Wito umetolewa kwa kwa wakaizi wa Mwanza na wilaya zake kuamka, kufumbua macho na kuona umuhimu wa huduma hii, kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wake utakao fanyika rasmi tarehe 29April 2014 katika viwaja vya Hospitali ya mkoa Sekoutoure.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.