ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 29, 2014

WABUGE MPINA NA KIRIGINI WAGAWA PIKIPIKI 25 ZENYE THAMANI YA MIL 55 KUIMARISHA UTEKELEZAJI ILANI CCM MEATU.

Mbunge wa Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina akikabithi fotokopi za kadi za pikipiki 25 na funguo za pikipiki pikipiki hizo kwa Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu Hilda Lucas Kapaya. Pikipiki hizo 25 zenye thamani ya sh milioni 55 zitagawiwa kwa Makatibu Kata wa CCM kwenye Kata 25 za Wilayani humo kwa ajili ya kuimarisha Chama na kuboresha utoaji wa huduma na taarifa kwa wakati.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Rosemary Kiligini ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu na Mjumbe wa Kamati ya Siasa wilayani humo, akikabithi kadi halisi za umiliki wa pikipiki 25 kwa Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu Hilda Lucas Kapaya ili zihifadhiwe Ofisi kuu kwaajili ya usalama.
Pikipiki 25 zilizo kabidhiwa.
Naye Katibu wa CCM wilayani Meatu, Jonathan Mabiha akipokea msaada huo, pamoja na kuwapongeza Kiligini na Mpina, alisema kuwa zitasaidia kuimarisha na kuboresha utendaji wa kila siku wa Chama na kuwataka Makatibu wake wazitumie kwa kuzingatia matumizi bora na sheria za usalama barabarani.
Ni pikipiki mpya 25 aina ya Fekon, zenye thamani ya shilingi milioni 55.
Kwa umakiiini wakisikiliza yanayojiri.
Rangi ya chama imehusishwa.
Baadhi ya Makatibu Kata kutoka kata mbalimbali wilayani Meatu wakiwa katika zoezi la majaribio ya Pikipiki walizokabidhiwa kwa ajili ya kuimarisha Chama na kuboresha utoaji wa huduma na taarifa kwa wakati.
Waheshimiwa meza kuu nao walipata fursa kujaribu ubora wa pikipiki hizo.
Pikipiki hizo 25 zenye thamani ya sh milioni 55 zimegawiwa kwa Makatibu Kata wa CCM kwenye Kata 25 za Wilayani humo kwa ajili ya kuimarisha Chama na kuboresha utoaji wa huduma na taarifa kwa wakati.
Sehemu ya makada pamoja na makatibu kata wa CCM wilaya ya Meatu waliohudhuria makabidhiano hayo ambapo awali kabla ya tukio hilo  walishiriki semina ya kuwajengea uwezo wa majukumu yao ya siasa.
Engo nyigine ya washiriki.
MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina ambaye pia ni Mjumbe CCM wa Kamati ya Siasa mkoani humo amebeza wanasiasa waongo na wenye kuwahadaa  wananchi na wakiwachonganisha na viongozi wa serikali.


Mpina alisema hayo juzi, wakati akizungumza na viongozi wa CCM ngazi ya Mkoa wa Simiyu, Wilaya ya Meatu na wanachama  kwenye hafla fupi ya kukabidhi Pikipiki 25 zilizotolewa na Mfadhili mmoja (Hakumtaja) kwa kushirikiana nayeye na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Rosemary Kiligini ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu na Mjumbe wa Kamati ya Siasa wilayani humo.

Pikipiki hizo 25 zenye thamani ya sh milioni 55 zimegawa kwa Makatibu Kata wa CCM kwenye Kata 25 za Wilayani humo kwa ajili ya kuimarisha Chama na kuboresha utoaji wa huduma na taarifa kwa wakati.

Mbunge Mpina, alimuonya Mbunge wa Jimbo la Meatu Meshack Opurukwa, kuacha tabia ya kukodi watu na kuwatukana viongozi wa CCM matusi, kusema uongo kwa wananchi pamoja na kupandikiza chuki kwa vijana wa CCM na Vyama vya Upinzani jambo ambalo linaweza kuleta machafuko na vurugu. 
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.


Aidha alieleza kwamba,  wanasiasa hao waliaminiwa na wananchi wakitarajia kuwa watakuja na kitu fulani cha kuwasaidia ikiwemo kuwatatulia keroa za maji, barabara, kuongeza madarasa na zahanati lakini matarajio hayo yameyeyuka baada ya kuonekana ni wababaishaji na waongo.

“Sote tunatambua kuwa wananchi wa jimbo la Meatu wanazo kero nyingi lakini Mbunge wao na wanasiasa wenzake waongo, hawaonekani, kazi yake ni ugomvi na kukodi watu kuja kutukana viongozi wa serikali na CCM, mfikishieni salamu zake, ajiandae kufungasha virago 2015.” Alisema Mpina.

Mpina ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kisesa wilaya ni Meatu, alisema mbunge mwenzake amesahau kazi aliyotumwa na wananhi wake na badala yake anaendesha porojo, uongo na kugombanisha vijana wa CCM na vyama vingine wawe maadui.

“CCM ina viongozi mashine na wenye sifa za kuwaongoza na kuwatumikia wananchi lakini huyo Mbunge mwezanagu, toka ameingia madarakani anaendesha siasa za chuki na matusi wakati anashindwa hata kuwaombea chakula cha msaada wananchi walioathilika na ukame katika baadhi ya maeneo ya jimbo lake.” Alieleza.

Mjumbe mwingine wa Kamati ya siasa ya wilaya hiyo, Rosemary Kiligini ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum mkoani Mara na Mkuu wa wilaya ya Meatu, alisema pikipiki hizo zimetolewa na mfadhili mmoja wa Chama (hakumtaja)baada ya yeye na Mpina kupeleka kilio cha Makatibu hao cha kutokuwa na vitendea kazi.

“Tunamshukuru mfadhili wetu aliyejitokeza kutuwezesha kununua pikipiki hizo 25 aina ya FEKON, zenye tahamani y ash milioni 55, ili kuwarahisishia Watendaji wa Chama Katani kuwasilisha taarifa na kuwafikia wanachama kwa wakati.” Alieleza.

Alitamba kwamba, serikali ya CCM ipo kikazi zaidi kutekeleza Ilani yake ili wananhi wapate maendeleo, wakati wapinzani wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi, ndiyo maana wamekuwa wakiwahamasisha vijana na wananchi kwa maneno ya uongo na uchochezi ili Taifa lisambaratike.

Kirigini alitoa wito na kuwaasa Makatibu Kata hao kutozitumnia nyenzo hizo kwa biashara ya bodaboda na kuzikodisha kinyemela kubeba mizigo kwani itakuwa kinyume na matarajio ya mfadhili waoa anayetaka Chama kiimarike na kuwang’oa wapinzani maana ni wababaishaji.

Naye Katibu wa CCM wilayani Meatu, Jonathan Mabiha akipokea msaada huo, pamoja na kuwapongeza Kiligini na Mpina, alisema kuwa zitasaidia kuimarisha na kuboresha utendaji wa kila siku wa Chama na kuwataka Makatibu wake wazitumie kwa kuzingatia matumizi bora na sheria za usalama barabarani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.