Meneja wa TRA mkoa wa Mwanza akifungua Semina ya na Waandishi wa habari juu ya ufafanuzi wa Mashine za Kielektroniki zinazotumika kukusanyia Kodi ya Mapato nchini iliyofanyika jana jijini Mwanza. |
Matokeo ya Utafiti, Changamoto na Utatuzi ni masuala yaliyo jadiliwa hapa. |
Konjes Mramba mwandishi wa habari toka gazeti la Raia Mwema akiuliza swali. |
Baadhi ya wafanyabiashara waaminifu wamewalalamikia wateja wao kutokuwa na utaratibu wa kuchukuwa risisti licha ya wafanyabiashara hao kuziandika mara baada ya mauzo. |
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imekamilisha mchakato
wa kufunga mita kwenye Mashine za kujazaia mafuta kwenye magari katika vituo
vyote ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi uliobainika kufanywa na wamiliki wa vituo
vya mafuta hapa nchini.
TRA pia imetoa Mashine mpya ya kukusanya Kodi ya
Mapato kwa wasafiri wa Ndege, Meli na
Mabasi ambayo awali yalikuwa na msamaha ikiwa ni pamoja na kuanza kutekeleza
Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) Cap 148, Sheria ya Kodi ya Mapato (Cap 332), Kanuni ya
VAT 2010 na Kanuni ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2012.
Hayo yalisema na Afisa Mwandamizi Mkuu wa Elimu wa TRA
nchini, Bw. Hamis Lupenja, wakati wa Semina na Waandishi wa habari juma hili
jijini mwanza, alipokuwa akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari
waliohudhulia na kutolea ufafanuzi wa Mashine za Kielektroniki zinazotumika
kukusanyia Kodi ya Mapato nchini.
Lupenja alizitaja Mashine hizo kuwa ni Printa za
Kosi za Kielektroniki za Kodi (EFP) ambayo itatumika kwa wafanyabiashara wa
rejareja wa maduka yote Makubwa, Vituo vya mafuta, Ofisi za huduma ya usafiri
wa Ndege, Meli, Treni na Mabasi na Feri watakaotumia mtandao na Rajesta za Kodi
za Kielekitroniki (ETR) itatumiwa na wafanyabiashara wa rejareja wa maduka
yanayotoa stakabadhi za mkononi.
Mashine nyingine aliitaja ni Mashine za Alama za
Kodi (ESD) ambazo zitatumiwa na wafanyabiashara maalumu katika utoaji wa sitakabadhi
ambazo zinauwezo wa kuratibu shughuli za kibiashara katika mtandao huo na
kuifanya Komputa kutokuwa na uwezo wa kutunza (Save) au kuchapa (Print) taarifa
yoyote bila idhini ya Mashine yenyewe.
Bw. Lupenja alieleza kuwa hivi karibuni TRA
itaendesha zoezi la kuhakiki wafanyabiashara ambao hawajanunua Mashine hizo
kutokana na muda wa kufanya hivyo uliokuwa umetolewa kuisha tangu Januari mwaka
huu ili kuwapatia Notice na wakiendelea kukaidi basi hatua kali za kisheria
kuchukuliwa ikiwemo adhabu au kufungiwa biashara yake kwa ukwepaji kulipa kodi.
Aliongeza kuwa kufatia mgomo uliofanywa na baadhi ya
wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali mikoani hapa nchini ikiwemo jijini
Mwanza, umepunguza kasi ya ufanisi wa ukusanyaji wa Mapato ya Serikali, hivyo
watakao kaidi kutumia Mashine za EFDs, ETRs, EFPs na ESDs wataangukiwa kwenye mkono
wa sheria kwa wanaopinga matumizi yake na kuidhoofisha serikali katika mapato.
“Suala la matumizi ya EFDs ni la kisheria, hakuna
sheria ya Kodi inayosema ugome na kuandamana hivyo matumizi ya mashine hizo
yataendelea kubaki kisheria isipokuwa panapoonekana pana tatizo tutakaa pamoja
na kuzungumza.” alisema Afisa huyo.
Alifafanua kwamba, baadhi ya wafanyabiashara
walioshiriki kwenye migomo hiyo walifata mikumbo kwa kutokujua au kutumiwa
maksudi na wachache wasiotaka kulipa kodi lakini hawahusiki na mpango wa awamu
ya pili ya matumizi ya EFDs kutokana na mauzo yao kwa mwaka kutozidi sh milioni
14.
Awamu ya kwanza ya matumizi ya EFDs ilianza Julai
2010 kwa wafanyabiashara waliokuwa wamesajiriwa kulipa VAT na awamu ya pili
iliyoibua migomo na maandamano imeanza Mei 2012 kwa wote wasiosajiriwa na VAT,
wanaouza zaidi ya kiasi hicho kwa mwaka (milioni 14).
“Awamu hii ya pili haiwahusu wafanyabiashara ndogondogo
(machinga) mamalishe, washinaji nguo, viatu na wauza mboga, matunda na wenye biashara ndogondogo zote na wanaouza
chini ya shilingi milioni 14 kwa mwaka, lakini ndio wengi wao walioshiriki
kwenye maandamano hayo, pengine kwa kutoelewa au kutumiwa.” Alieleza Lupenja.
Kwa mujibu wa takwimu zilizoelezwa na Afisa wa Elimu
kwa Mlipa Kodi wa TRA Bw.Yustas Augustino alisema kwamba Mkoa wa Mwanza , hadi
sasa una wafanyabiashara zaidi ya 6500 waliosajiriwa kwa matumizi ya EFDs
wakiwemo 1,500 waliosajiriwa awamu ya kwanza na awamu ya pili wakiwa ni 5,000.
Maofisa hao waliwataka wafanyabishara wawe wazalendo
na kutokwepa matumizi ya mashine hizo kama ambavyo baadhi ya watu wanavyozusha
kuwa zinawanyonya. EFDs zinatoa uhakika wa usalama wa taarifa za biashara,
hutoa haki katika tathmini ya kodi na kurahisisha kufanya makadilio yaliyo
sahihi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.