FAINALI ZA SAFARI HIGHER LEARNING POOL COMPETITION KUFANYIKA MAI 3 NA 4,2014 MKOANI KILIMANJARO.
Dar es Salaam leo; Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia Bia yake ya Safari Lager leo wametangaza siku ya kufanyika kwa fainali za kitaifa za mashindano ya mchezo wa Pool ujulikanao kama “Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2014”.
Fainali za Kitaifa ziatarajiwa kufanyika Mai 3 na 4 mwaka huu Moshi Kilimanjaro katika Ukumbi wa Aventure kwa kukutanisha mabingwa wa vyuo kwa kila mkoa kutoa katika mikoa 8 ya nchini Tanzanzania ambako mashinadano haya yalianzia katika ngazi za mikoa.
Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alikipongeza chama cha Pool Tanzania (TAPA) kwa kuendesha mashindano vizuri katika ngazi ya mikoa na hatimaye kupata mabingwa wa kila mikoa watakaopeperusha bendera za mikoa yao kwenye fainali za kitaifa.
Aidha Shelukindo alivipongeza vyuo vilivyofanikiwa kufika fainali na kuwaomba kuwa watulivu katika harakati zote za mchezo wa kutafuta bingwa mpya wa kitaifa 2014 baada chuo cha CBE kunyanganywa ubingwa katika ngazi ya mkoa jijini Dar es Salaam ambao ndio walikuwa mabingwa watetezi wa 2013.
“Imebainika duniani kote kwamba michezo inanguvu ya kuwaleta watu pamoja, kufundisha na kukuza vipaji na vile vile kujenga afya bora. Tunajivunia kwa mara nyingine kuwa wadhamini wa mchezo huu, ambapo wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali watakutana na kushindana kwenye mazingira mazuri”, alisema Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo .
- Zawadi za mwaka huu ngazi ya Taifa ni kama ifuatavyo;
- Teams;
- Mshindi wa kwanza – 2, 500,000
- Mshindi wa pili – 1,500,000
- Mshindi wa tatu – 1,300,000
- Mshindi wan ne – 1,000,000
- Walioshindwa robo fainali wane – 500,000 Kila timu.
- Singles;
- Wanaume; Mshindi wa kwanza – 300,000
- Wanaume; Mshindi wa pili – 200,000
- Wanaume Mshindi wa tatu – 150,000
- Wanaume Mshindi wan ne – 100,000
- Wanawake; Mshindi wa kwanza – 200,000
- Wanawake; Mshindi wa pili – 150,000
- Wanawake Mshindi wa tatu – 100,000
- Wanawake Mshindi wan ne – 50,000Nae Katibu wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga aliipongeza Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kwa kuendelea kudhamini mashindano ya Pool Vyuoni na Taifa kwa ujumla ikiwa ni mwaka wa sita sasa.Aidha alivitaja Vyuo vilivyofanikiwa kufika fainali kuwa ni1.IRINGA - RUCCO2.MBEYA - MZUMBE3.MOROGORO - SUA4.MOSHI - MUCCOBS5.DODOMA - ST.JOHN6.ARUSHA - IAA7.MWANZA - BUGANDO8.DAR ES SALAAM - ARDHINae mratibu wa fainali hizo, Peter Zacharia alisema maandalizi mpaka sasa yako tayari,Hoteli za kufikia wanafunzi zimeshaandaliwa ikiwa ni pamoja na usafiri wao.Peter alimaliza kwa kutaja burudani za mwaka huu zitasindikizwa na burudani ya Muziki wa dansi kutoka kwa Malindi Bandi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.