ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 31, 2014

UN YAZIIMARISHA CLUB ZAKE (UNA) KANDA YA ZIWA KWAAJILI YA KUFIKIA MALENGO YA MILLENIA 2015.

Afisa habari wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Usia Nkhoma (wa pili kutoka kushoto) akiwa na mkutubi wa shirika hilo Bi. Hariet Macha (katikati) wakikabidhi vitabu  na machapisho mbalimbali ya taarifa kwaajili ya maktaba ya chuo cha CBE Mwanza ili wanafunzi wapate kusoma na kujua habari za Umoja wa Mataifa. Kushoto ni  Mr. Kimambo ambaye ni mkurugenzi wa CBE, na wa kwanza kulia ni Afisa rasilimali watu CBE Mwanza
Ni machapisho yenye taarifa, katiba, uchambuzi na ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kwaajili ya Club ya vijana wa Umoja wa mataifa (UNA) pamoja na wanafunzi mbalimbali ambao wanahitaji kuujua umoja huo.
Maelekezo mafupi juu ya machapisho.
Kuanzishwa kwa Clubs na Chapters ni mwendelezo wa kufungua fursa na mwongozo kwa vijana kujua majukumu yao katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya millenia.
Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania bi Usia Nkhoma Ledama alisema takwimu zinaonesha kuwa asilimia 52 ya vijana wa kike umri wa miaka 18-14 wameanza kufanya ngono na na asilimia 7 kwa wenye miaka 15-19 wanafanya ngono na wanamme wanaowazidi umri miaka 10 zaidi, huku vijana wa kiume wakidaiwa kuanza kufanya ngono wakiwa na umri wa miaka 20, akatumia fursa hiyo kuwataka vijana kuepuka ngono kwani wakindekeza ngono UKIMWI upo na hawataweza kutimiza ndoto zao.
Wanafunzi wa Chuo cha Biashara CBE Mwanza wakimsikiliza kwa makini Bi. Usia ambaye aliongeza kuwa Umoja wa Mataifa haupo tayari kuendelea kuona vijana wakishindwa kutimiza malengo yao.
Ni vijana wa CBE Mwanza wakiwa katika hali ya umakini ndani ya ukumbi wa Teknolojia chuoni hapo ambapo wameaswa kutumia vyema fursa mbalimbali zinazotolewa na Umoja wa mataifa hapa nchini kwa mustakbari wa maisha yao, lakini pia wazazi na walezi wa wanafunzi wamepewa angalizo kujenga tabia ya kufuatilia mienendo ya watoto wao na kuwasaidia ili kuwafanya wapende elimu ili kufikia malengo ya millenia.
Mkutubi wa Umoja wa Mataifa Bi. Hariet Macha akiweka msisistizo juu ya msingi wa kujisomea ambao ndiyo silaha ya mafanikio, msingi ambao hujengwa katika umri wa ujanani.
Mratibu wa Asasi ya Umoja wa Mataifa Kanda ya Ziwa Mr. Moses Mongo alizungumza na wanachuo wa CBE Mwanza, kwa kuitambulisha asasi hiyo akisema kuwa ilianzishwa mnamo mwaka 1964 kote duniani ikiwa na malengo ya kuleta mabadiliko kwa kutumia nguvu za vijana walio wengi katika mataifa mbalimbali ulimwenguni.
Mweyeji wa UNA CBE Mwanza.
Lengo kuu la ziara hii ni kuhamasisha  uanzishwaji wa klabu za Vijana za Umoja wa Mataifa na kutoa elimu kuhusu shughuli za umoja huo ambapo timu ya watu sita imewatembelea vijana wa shule za msingi, sekondari na vyuo mbalimbali kanda ya ziwa kuwaelimisha kuhusu ajenda za Umoja wa mataifa kama vile changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi, umaskini, ajira, afya ya uzazi, UKIMWI, mimba za utotoni, elimu n.k ili vijana wazifanyie kazi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.