Mstahiki wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula akiwa kikaoni na Balozi mdogo wa China nchini Li Xuhang na ujumbe wake ofisini kwa Meya alipotembelea Jiji la Mwanza |
Mstahiki Meya Mabula akifafanua jambo kwa Balozi mdogo wa China nchini Li Xuhang |
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanislau Mabula (Diwani wa Kata ya Mkolani) akiwa ni Meya wa 10 tangu kuanzishwa Mji na Jiji hili la Mwanza |
Meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula (kushoto) akiwa na Balozi mdogo wa Canada nchini alipomtembelea ofisini kwake Jijini Mwanza. |
Mchumi wa Jiji la Mwanza Joseph Kashushula (kulia) akiwa na Balozi mdogo wa Canada ofisini kwa Meya wa Jiji la Mwanza kwa picha ya kumbukumbu baada ya kutembelea Jiji hilo. |
Na PETER FABIAN (gsengoblog)
UBALOZI wa China umekusudia kuwaleta wafanyabiashara
na makampuni kutoka nchini humo kuja kuwekeza Jiji la Mwanza kutokana na
rasilimali zilizopo ikiwemo maeneo ya uwekezaji.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Msaidizi wa Balozi
wa China nchini Bw. Li Xuhang aliyeongoza ujembe mdogo wa china walipotembelea
Jijini Mwanza na kukutana na uongozi wa Jiji la Mwanza ambapo walikutana na
Meya wa Jiji Bw.Stanislaus Mabula na Mkurugenzi wa Jiji hilo Bw. Alfa Hassan
Hida kwa mazungumzo jinsi ya kushirikiana katika Nyanja mbalimbali.
Bw. Xuhang alisema kwamba lengo la ujumbe huo
kubisha hodi kwa uongozi wa Jiji la Mwanza ni kudumisha ushirikiano katika
Nyanja za Uchumi na Biashara kwa miaka hamsini tangu kuwa na mahusiano na Taifa
la China ambapo pia jina la Jiji la Mwanza linao umaarufu nchini china kutokana
na kuwa Kitovu cha nchi za Maziwa Makuu sanjari na kuwepo rasilimali na maeneo
ya uwekezaji.
“Ni fursa ya pekee kwa wafanyabiashara na makampuni
ya nchini kwangu kuchangamka na kuja kuwekeza Jiji la Mwanza ambapo kwa upande
wa Viwanda mbalimbali vya kutengeneza bidha za vyombo vya ndani, nguo, ofisini
na mitambo mbalimbali ikiwemo ya ujenzi na ujenzi wa majengo marefu ya kitega
uchumi ikiwemo miundombinu ya barabara” alisema
Bw. Xuhang aliongeza kuwa wawekezaji wa china
wakitumia fursa hii kuja kuwekeza hakika Jiji la Mwanza litakuwa mfano na
litaongeza kasi ya ukuaji wake kutokana na kuwa na maeneo ya uwekezaji,
rasilimali na maeneo mengi ya vivutio mbalimbali vya utalii likiwemo ziwa
Victoria na kusaidia upatikanaji wa ajira kwa wananchi wakazi wa Jiji hili na
Mkoa wa Mwanza.
“Nimefurahi kupatiwa taarifa za kuwepo wananchi
wenzangu kutoka nchini china wapatao 200 wanaojishughulisha na miradi
mbalimbali ikiwemo ujenzi wa majengo marefu, barabara, zana za kilimo, uvuvi na
biashara mbalimbali jambo ambalo litaongeza chachu ya kuwahamasisha wenye uwezo
kuja kuwekeza zaidi” alisisitiza Balozi huyo mdogo.
Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Bw. Stanislaus
Mabula kwanza aliupongeza Ujumbe huo wa China na kuonyesha ushirikiano na Jiji
la Mwanza kwa muda mrefu na kutaka udumishwe na kuendelezwa na kuenziwa ili
kutoa fursa kwa kila upande kubadilishana uzoefu na kufahamiana zaidi ili
kuweka mahusiano ambayo itakuwa chachu ya kuwavutia wawekezaji.
Mstahiki Mabula alisema kwamba katika bmazungumzo ya
kina na ujumbe huo uongozi wa Jiji la Mwanza umekusudia kuushawishi ujumbe huo
kuendelea kulisaidia Jiji hili katika sekta na Nyanja mbalimbali za maendeleo
na kiuchumi pamoja na kulipatia vitendea kazi (mitambo) kwa ajili ya barabara
za Jiji, uzoaji taka na usafi wa mazingira, redio ya jiji, idara ya ardhi na
mipango miji na vifaa vya Teknolojia, ulinzi na mawasiliano.
“Tunao ushirikiano wa muda mrefu kwa miaka hamsini
(50) sasa na wenzetu hawa wa china ambapo katika uhusiano wetu kuna Kampuni
ya China Railway Jianchang Engineering
Co.(T) Ltd (CRJE) inajenga jengo la Kituo cha Kibiashara maeneo ya Ghana ambalo
Jiji limeingia ubiya ya LAPF ambapo pia tunayo mahusiano kwa miaka 50 na Mji
rafiki lijulikanalo Yungup District uliopo Jiji la Shanghai nchini China ambapo
tangu mwaka 2008 mahusiano yaliboreshwa.
Meya pia aliomba ujumbe huo kwa kushirikiana na
serikali ya china kujitokeza kulisaidia katika ujenzi wa soko la kisasa la
samaki na nafaka linalotaraji kujengwa maeneo ya Kata ya Mkuyuni ambalo liko
katika mpango wa Jiji kuwa na kitega uchumi na litakalotoa huduma kwa mikoa ya
jirani na wakazi wa Mkoa wa Mwanza ikiwa ni chanzo kipya cha kuliingizia jiji
mapato zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Hida alimwomba
Balozi huyo mdogo na ujumbe wake kulisaidia jiji katika sekta ya Elimu katika
ujenzi wa Maabara katka shule za sekondari za Kata zote 12, Makitaba na kuzipatia madawati ya kutosha ili
kuondokana na tatizo hilo ambalo limekuwa kero kwa wazazi kutakiwa kuchangia
gharama za upatikanaji wake.
Mkurugenzi Hida pia alisema Ubalozi huo ufikishe
ombi la Jiji kwa serikali ya china kulisaidia jiji kuboresha vifaa vya
kuboresha na kurusha matangazo ya redio yake na kulipatia pia mitambo ya kisasa
ya kuanzisha Televishion (TV) yake kwa ajili ya kutoa elimu na matangazo
mbalimbali kwa jamii juu ya shughuli za kijami zinazofanywa na Jiji katika
maeneo ya kata zake 12.
“Tunaimani na wenzetu hawa kutusaidia kwa kiasi
furani kutokana na mahusiano yetu kwa miaka hamsini (50) kwani ikitekelezwa
hakika jiji la mwanza litakuwa na hadhi ambayo itawavutia wawekezaji wengi
zaidi kutoka mataifa ya China (Asia), Ulaya na Amerika kutokana na kuwepo
maeneo ya uwekezaji na miundombinu iliyo rafiki kwa wawekezaji” alisema.
Wito wangu kwa wananchi wa Jiji la Mwanza kuwa
tayari kuwapokea wawekezaji kutoka mataifa ya china na mataifa mengine na
kudumisha usafi wa mazingira yetu pamoja na kuwa tayari kushirikiana na
wawekezaji kupitia fursa na rasilimali zilizopo katika sekta mbalimbali za
kiuchumi na maendeleo ili kulipaisha kimataifa jiji hili lilio kitovu cha nchi
za Maziwa Makuu na Kanda ya ziwa
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.