TOTAL
YAZINDUA AWANGO KUMALIZA TATIZO LA UPATIKANAJI WA UMEME KWA WATU WA KIPATO CHA
CHINI TANZANIA
Dar es salaam, 27 Februari, 2014.
Tatizo
la ukosefu wa nishati ya umeme kwa jamii ya watu wa kipato cha chini Tanzania linatarajiwa
kufikia kikomo, baada ya TOTAL, moja ya kampuni inayoongoza katika biashara ya
nishati duniani, kupitia mradi wa ‘Total Access to Solar (TATS)’ kutambulisha
aina mpya ya bidhaa za taa pamoja na vifaa vya kuchajia simu vinavyotumia
nishati ya jua vyenye kudumu na vinavyopatikana gharama nafuu nchini Tanzania.
Total
Access to Solar (TATS) ni mradi ulioanzishwa na TOTAL mwaka 2010, ukiwa na
shabaha ya kuhakikisha upatikanaji wa suluhisho la vifaa vya nishati mbadala katika
soko la dunia kwa matumizi ya kijamii na kiuchumi ikilenga jamii ya kipato cha
chini. Mradi wa TATS unaendana na mlengo
wa kibiashara wa TOTAL ambao ni “Kuwajibika katika upatikanaji wa nishati
kwa watu wengi zaidi kadri inavyowezekana, na kupambana na mahitaji ya dunia”
Miradi ya TATS yote inalenga katika
kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika shughuli za kijamii na kiuchumi kwa
kutumia nishati itokanayo na vyanzo vya uhakika vikiwemo Jua, Gesi, Mafuta na
mabaki ya plastiki. Kwa kugundua mahitaji makubwa ya nishati mbadala kwa
Watanzania, TOTAL Tanzania kupitia TATS imezindua rasmi bidhaa mpya zilizo
chini ya mradi wa AWANGO, zikiwa ni maalum kwa ajili ya jamii ya Kitanzania.
AWANGO ni mradi unaoleta
bidhaa zinazotumia nishati ya jua kuweza kuzalisha umeme. Lengo kuu ni
kuwezesha matumizi ya nishati ya jua kama suluhu itakayowezesha upatikanaji wa
umeme wa uhakika na nafuu kwa jamii ya watu wa kipato cha chini wanaoishi
vijijini na pembezoni mwa miji.
Kabla ya kuzinduliwa
Tanzania, mradi wa AWANGO ulishaanza kufanya kazi katika nchi nne duniani huku ukifanyiwa
majaribio kwa zaidi ya mwaka mmoja. Baada ya mafanikio katika nchi za Cameroon,
Indonesia, Kenya na Jamhuri ya Kongo, zaidi ya taa 125,000 na vifaa vya Jua
viliuzwa, baadae mradi huu ulikua na kufikia nchi nyingine nane.
Akihutubia wakati wa uzinduzi wa
AWANGO, mgeni rasmi Mhe. Prof. Sospeter Muhongo, ambae ni Waziri wa Nishati na
Madini aliwapongeza TOTAL kwa kusaidia kutatua kero ya upatikanaji wa nishati
ya uhakika nchini, “kwa niaba ya Serikali, nawapongeza
TOTAL kwa kwenda mbali zaidi na kuona uhitaji wa wananchi wetu juu ya
mabadiliko na kupiga hatua ya kutatua tatizo upatikanaji wa nishati”.
Kwa kuzingatia mahitaji makubwa
ya umeme yanayoongezeka kila siku, bidhaa za AWANGO zimetengenezwa kukabiliana na
ongezeko hili. Ufanisi, unafuu na kudumu kwa muda mrefu ndio sababu kubwa zinazofanya
ya vifaa vya AWANGO kuwa tofauti na vifaa vingine vilivyozoeleka kutumika na
jamii ya kipato cha chini.
Akizungumza juu ya upatikanaji wa
bidhaa hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa TOTAL Tanzania Bw. Stephane Gay alisema
kwamba bidhaa hizi zitapatikana katika vituo vyote vya mafuta vya TOTAL vilivyopo
takribani mikoa yote ya Tanzania, lakini pia kampuni hiyo itashirikiana na
wadau wa maendeleo zikiwema asasi za kijamii katika usambazaji, ikiwa ni
Dhamira ya kupeleka bidhaa za AWANGO nchi nzima.
Ikiwa kama bidhaa ya kibiashara
inayosaidia jamii, AWANGO imejidhatiti katika kutoa huduma bora na ufanisi mkubwa
kama ilivyo TOTAL. Mradi huu unatazamiwa kuwa na matokeo matatu katika njia
tofauti za Kiuchumi, kijamii na kulinda mazingira. Shabaha kubwa ni kumpa
Mwananchi wa kipato cha chini nguvu ya kujikwamia kimaendeleo kijamii na
kiuchumi.
KUHUSU
TOTAL
TOTAL Tanzania Ltd ni kampuni inayojishughulisha
na usambazaji wa bidhaa za nishati ya petroli na mafuta ghafi. Kampuni hiyo
ilianzishwa mwaka 1969 ikiwa na makao makuu yake Dar Es Salaam, TanzaniaTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.