ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 5, 2014

MGOGORO WA ARDHI UZIDHIBITIWE KABLA YA KULETA MAAFA BWIRU MWANZA.

MGOGORO WA ARDHI UZIDHIBITIWE KABLA YA KULETA MAAFA BWIRU MWANZA.

Na .Peter Fabian.                                                                    05/03/2014
MWANZA.

WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Bwiru Manispaa ya Ilemela wanatuhumiwa kupora maeneo ya shule na kujigawia viwanja na kujenga makazi yao binafisi ndani ya maeneo ya shule hiyo kinyume na taratibu na sheria za Ardhi za Manispaa ya Ilemela na kupelekea wananchi kulalamikia kuporwa maeneo yao na walimu hao Jijini hap.

Hatua hiyo imelalamikiwa na wananchi wa maeneo ya Bwiru Mnalani na jirani na shule ya sekondari hiyo baada ya hatua ya walimu hao kuanza udanganyifu na kuwatoa wanafunzi kwenye vipindi vya masomo darasani na kuwatuma kuvamia maeneo ya wananchi wa maeneo hayo ya jirani na kufanya uhalibifu kwa kung’oa nguzo za alama na kusogeza mipaka zaidi.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa baadhi ya wananchi hao akiwemo Patrick Mlelwa aliyevunjiwa nguzo sita alizokuwa amezungushia eneo lake na kuchukuliwa na wanafunzi hao waliodaiwa kutumwa na Mkuu wa Sekondari hiyo Mwl. Hadja Mpiwa na Msaidii wake Mwl. Cool kwa lengo la kupora maeneo ya wananchi kwa kisingizio cha kuwa ndani ya eneo la shule.

“Leo asubuhi nilipewa taarifa na baadhi ya watu waliokuwa wakipita katika jirani na eneo la kiwanja changu ambapo walinieleza kuwa kuna wanafunzi wasichana wa sekondari ya Bwiru wanang’oa nguzo nilizozungushia eneo langu na kuonyesha mpaka, niliofika nilikuta wameisha ondoka na nguzo sita basi sikuwa na la kufanya zaidi ya kutoa taarifa kwa balozi wa eneo letu” alisema Mlelwa.

Mwananchi mwingine Lazaro Magera alieleza kwamba kumekuwepo na uvamizi wa maeneo yao na uharibifu wa mali unaofanywa na wanafunzi hao kwa madai ya kuagizwa na walimu wao kuwa ni kuhakikisha wanalinda mipaka ya shule yao na kuwaondoa waliovamia maeneo yao ya sekondari hiyo ili kuwakomesha kujichukulia maeneo ya kwa mujibu wa kuelezwa na walimu wao.

“Tuliwahi kutachia maeneo ya kujenga shule ya sekondari ya Mwinuko ya Kata ya Pasiansi na hata hiyo ya Bwiru Wasichana lakini baadhi ya Vigogo, Madiwani, Maafisa Ardhi wa Jiji na Walimu waliyachukua na kujenga makazi yao na wengine kuuza kwa watu wengine leo tena wanakuja na mbinu zile zile sasa hatukubali kunyanyaswa tutatetea haki yetu kwa nguvu zote” alisisitiza.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Bwiru Magharibi Agnes Kingu alithibitisha kuwepo mgogoro huo kwa muda mrefu ambao unatokana na wananchi kuwa na maeneo yuao lakini Halmashauri ya Jiji wakati huo na sasa Manispaa ya Ilemela kushindwa kuyatambua na kuwapimia na sasa Manispaa nao kushindwa kuyapima ili kuwamilikisha kisheria wananchi hao jambo ambalo walimu nao wanadai ni maeneo ya shule yalivamiwa.

Kwa upande wake Mkuu wa sekondari hiyo Mwl. Mpiwa alipoulizwa kusiana na tukio la kuwatumia wanafunzi kung’oa nguzo na kuzichukua kwa madai ya kuwaondosha waliovamia maeneo ya shule aliambia kwa njia ya simu yake ya mkononi kuwa yeye si msemaji na atafutwe Mkurugenzi wa Manispaa Zuberi Mbihana kwa vile shule hiyo iko chini ya mamlaka yake.

“Sina cha kukujibu lakini mimi siyo mwenye mamlaka ya kulizungumzia suala hili kwani hata hao wananchi walivamia maeneo ya shule na hata Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Amina Masenza anatambua hilo na aliisha wahi kuja tukamuonyesha na aliwaamuru kupisha sasa kama wamekuja kushitaki kwenu mpigie DC akupe majibu mimi usinisumbue na kazi zangu” alisema kisha kukata simu.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mbihana alipotafutwa na mwandishi wa habari hii alikiri kuwepo kwa mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na viongozi wa shule hiyo na kupelekea kila upande kudai umevamiwa, kutokana na suala hilo kumladhimu Mkuu wa Wilaya kuingilia kati kwa kufika na kufanya mkotano na walimu na kuonyesha maeneo yaliyovamiwa.

“Halmashauri ya Manispaa imetuma timu ya wataalamu kwenda kuyahakiki maeneo hayo na kuyapima zoezi ambalo linaendelea kwa sasa na baada ya kukamilika tutawapatia taarifa na kitugani kimebainika hivyo wananchi watashirikiana na Maafisa Ardhi wetu kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa ili kumaliza mgogoro huo na kulidhiwa na pande zote mbili” alisema Mbihana kutumia simu yake ya kiganjani.

Mkutugenzi huyo aliongeza kuwa kufatia kuibuka kwa mgogoro huo ambao hata hivyo umedaiwa kuwa wa muda mrefu ni kuwasihi wananchi na walimu kuwaachia Maafisa ardhi kulishughulikia kwa kufanya upimaji na kisha tutatoa majibu na kuwahasa walimu kutowatumia wanafunzi kwenda kung’oa nguzo na vigigngi kwenye maeneo ya wananchi walio jirani na maeneo ya shule. 

“Walimu kutumia wanafunzi si jambo la busara kwani kunaweza kukatokea machafuko baina ya wanafunzi na wazazi wao na ikizingatiwa wale ni watoto wa kike hivyo tumeomba sana busara iwatangulie walimu na wananchi ili zoezi hili la kuhakiki lifanywe na maafisa ardhi wa Manispaa na hakuna dhuluma yoyote na hakika haki itatendeka tunaomba ieleweke hivyo”alisisitiza.

Katibu wa CCM Kata ya Pasiansi Consolata Faustine alisema kuwa kufatia mgogoro huo umekuwa na changamoto kubwa kwa viongozi wa Mashina, Matawi na Kata hiyo kufatilia kutokana na baadhi yao kumtuhumu Mkuu wa Wilaya kuwa anashirikiana na walimu wa shule ya Bwiru ili kuwasaidia kutaifisha maeneo yao kwa kutumia kivuli na kisingizio cha maeneo hayo kuwa sehemu ya shule.
“Wananchi ambao baadhi yao ni wanaccm zaidi ya mia mbili (200) wametishia kurudisha hadi Kadi za Chama (CCM) lakini tumewasihi kutofanya hivyo na badala yake tuwapatie nafasi wahusika kushughulikia suala hili na wito wangu kwa maafisa ardhi walishughulikie kwa umakini mkubwa na busara iwatangulie na hatua zichukuliwe kabla ya kuleta maafa” alisisitiza.

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Masenza akizungumza kwa njia ya simu yake ya mkononi alisema kuwa tayari kuna zoezi la kuhakiki na upimaji linaendelea kufanywa na maafisa ardhi baada ya kumweleza Mkurugenzi wa Manispaa kuwa kuna tatizo alishughulikie haraka hivyo tuwapatie muda na wakimaliza basi tutatolea taarifa kwa pande zote mbili zilizo na mgogoro huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.