ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 5, 2014

HIZI NDIZO BAA 5 ZILIZOTINGA FAINALI YA SAFARI NYAMA CHOMA MWANZA.

Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Ziwa, Erick Mwaye (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tukio la shindano la Safari Nyama Choma linalotarajiwa kufanyika jumapili ya wiki hii katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza. 

Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Ziwa, Erick Mwaye (kushoto) akimkabidhi mtangazaji wa Passion Fm Philbert Kabago, zawadi ya kinywaji na 'tooth stik mpya' zikiwa ndani ya mkebe mithili ya Safari ya kopo, zilizo buniwa kwa ajili ya shindano la Safari Lager Nyama Choma 2014.
Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Ziwa, Erick Mwaye (kushoto) akimkabidhi mtangazaji wa Radio Free Afrika Magasha, zawadi ya kinywaji na 'pama' kwa ajili ya shindano la Safari Lager Nyama Choma 2014.
Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Ziwa, Erick Mwaye (kushoto) akimkabidhi mtangazaji wa Metro Fm Alex Ngusa,  zawadi ya T'shirt na kinywaji kwa ajili ya kujiachia jumapili ya tarehe 9 Uwanja wa Furahisha kwenye shindano la Safari Lager Nyama Choma 2014.
Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Ziwa, Erick Mwaye (kushoto) akimkabidhi mtangazaji wa Barmedaz Tv,  zawadi ya Kofia na kinywaji kwa ajili ya kujiachia jumapili ya tarehe 9 Uwanja wa Furahisha kwenye shindano la Safari Lager Nyama Choma 2014.
Nkabaaa ni kofia aina ya pama na kinywaji. 
SAFARI LAGER YATANGAZA RASMI BAA 5 ZILIZOINGIA FAINALI KATIKA SHINDANO LA UCHOMAJI NYAMA MKOA WA MWANZA  KWA MWAKA 2014.
Mwanza, Jumatano 5 Machi 2014: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi majina ya Bar 5 yaliyofanikiwa kuingia fainali katika  shindano la uchomaji nyama kwa mwaka 2014 lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma Competition 2014”.

Shindano hili linalofanyika kila mwaka, linafanyika mwaka huu kwa mara ya saba mfululizo na litashirikisha mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Dar Es Salaam. 

Tangu lilipoanzishwa mwaka 2008, shindano hili limekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya Safari Lager kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na ushindi katika mkoa waliopo. Kwa mwaka huu baa 5, zilizopigiwa kura kwa wingi(Top 5, Bars) ni   Lunala Bar, Victoria Prince, Shooter’s Pb, Gemstone Bar na SD Executive. Jumla ya  Bar 45 zilipigiwa kura kwa Mkoa wa Mwanza.

Baa hizi zilizopata kura nyingi zaidi zitachuana kwa kuchoma nyama katika tamasha la wazi litakalofanyika katika viwanja vya Furahisha hapa jijini Mwanza zikikisindikizwa na burudani ya muziki wa Bendi ya hapahapa  Mkoani Mwanza ya Sebedaki (Wazee wa Sebene) .

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Ziwa, Erick Mwayela, alisema , “Lengo kuu la shindano la Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora katika uchomaji na utayarishaji wa nyama choma.

Tunahakikisha wachoma nyama katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma.

Alisema Fainali za Mashindano zitafanyika Machi 9, Mwaka huu katika Viwanja vya Furahisha kuanzia saa tatu asubuhi ambapo washindi watapewa zawadi kuanzia mshindi wa kwanza atakayejinyakulia Shilingi Milioni moja na Kikombe, mshindi wa pili Laki nane, Mshindi wa tatu Laki 6, Mshindi wa nne laki nne na Mshindi wa Tano shilingi laki mbili.

Bwana Erick  alimaliza kwa kusema kwamba, “Safari Lager tutaendelea kujitahidi kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora ya nyama choma pale wanapoihitaji. Tunawaomba sana washiriki kutumia vizuri elimu na uzoefu wanaopata ili kuongeza ubora wa utayarishaji wa nyama choma kwa wateja wetu. Mashindano haya ya Safari Lager Nyama Choma yatakosa maana sahihi endapo wachoma nyama watakuwa wanashiriki kwa lengo la kujipatia manufaa binafsi na kusahau yale yote waliyojifunza hadi mwaka mwingine”. Shindalo la mwaka huu linaongozwa na kibwagizo…. Bila Safari Lager, Nyama Choma haijakamilika!.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.