ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 26, 2014

MJUMBE WA NEC CCM TAIFA NA WAZIRI, SOFIA SIMBA MGENI RASMI KONGAMANO LA WANAWAKE SAUT MWANZA

Na PETER FABIAN.
MWANZA.                                                                    

WANAFUNZI wa Vyuo Vikuu kwa kushirikiana na Vyuo vingine wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Cha Mapinduzi (UWT) na wasio wanachama kushiriki Kongamano kubwa la kuadhimisha miaka 52 ya uhuru wa Taifa hili Machi Mosi Mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana Jijini hapa, Katibu wa UWT tawi la Kambarage Chuo Kikuu cha St. Agustine (SAUT) lililopo Malimbe Kata ya Mkolani Wilayani Nyamagana Jesca Mbogo alisema kuwa Kongamano hilo litafanyika siku ya Machi Mosi mwaka huu katika ukumbi wa Masista wa Kanisa Katoloki uliopo eneo la Malimbe Chuoni hapo.

Katibu Mbogo alieleza kwamba kongamano hilo litakaloshirikisha wanafunzi wote wa Vyuo Vikuu na vingine vilivyopo Mkoani humo ambao ni wanachama wa UWT na wasio wanachama kuadhimisha miaka 52 ya Uhuru na Maendeleo ya Mwanamke ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini ya mwanamke katika kujiletea maendeleo kwa kipindi hicho na kijacho.

“Kauli mbiu ya kongamano hilo ni ‘Miaka 52 ya uhuru na maendeleo ya mwanamke’ lengo ikiwa ni kuwakutanisha wanawake wasomi wa vyuo vikuu na vyuo vingine walio wanachama wa UWT na wasio wanachama Mkoani Mwanza kuadhimisha uhuru wa taifa hili na kufahamiana na kujadili maendeleo ya mwanamke na nini nafasi ya mwanamke katika kulitumikia taifa lake” alisema.

Katibu huyo, alifafanua kuwa kongamano hilo la kwanza kufanyika Mkoani Mwanza na kuhusisha waosomi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani humo lisitazamwe kwa jicho baya bali ni kuwasaidia wasomi hao kufanya tathimini yao jinsi ya mwanamke anavyopambana katika kujiletea maendeleo ndani ya taifa lake huru na kubadilishana uzoefu na majukumu ya uongozi ndani ya Umoja wa Wanawake (UWT).

Mbogo alisema kuwa kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika siku ya Machi Mosi mwaka huu kama ilivyopangwa na kuandaliwa na Tawi la UWT Kambarage kwa kushirikiana na UWT Mkoa wa Mwanza ambapo Mgeni rasmi wa kongamano hilo atakuwa Mwenyekiti wa UWT Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Sofia Simba ambaye pia ni Waziri wa Wizara ya Wanawake Jinsia na Watoto.

“Tayari Waziri Simba ameisha thibitisha kuwepo kama mgeni rasmi na maandalizi ya kongamano hilo yanaendelea na kwa kiasi hadi sasa yamekamilika kwa asilimia 90 tuko mbioni kukamilishka asilimia zilizobaki na sasa tumekwisha peleka taarifa (Baruaza mwaliko) kwenye Vyuo vikuu vya Umma, Mashirika, Taasisi na Binafisi lengo ni kuwapatia nafasi na kupatiwa ruhusa ya kuhudhulia kwa wanafunzi hao” alisema 

Katibu huyo ametoa wito kwa baadhi ya wafadhili wa kongamano hilo kuunga mkono wa dhati juhudi za UWT Mkoa na tawi la Kambarage ili kufanikisha, pia amewataka wanawake wote wasomi vyuo vilivyopo Mkoani Mwanza kujitokeza kwa wingi kushiriki kongamano hilo la siku moja la kuadhimisha miaka 52 ya uhuru wa taifa hili na maendeleo ya wanawake msomi walioko vyuo vikuu na vingine.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.