MBUNGE
wa Jimbo la Rorya Bw. Lamerck Airo amemvaa Mkuu wa Wilaya ya Rorya akimtaka
kuacha kuwasha kuwashutumu wanasiasa kuwa ndo wanakwamisha ukusanyaji wa mapato
ya Halmashauri ya Rorya na kuwakingia kifua wataalamu wanaofanya ubadhilifu wa
fedha za umma.
Mbunge
Airo alisema kuwa kitendo cha Mweka Hazina kufanya ubadhilifu wa milioni 111.7
na kuhamishwa huku baadhi ya Madiwani 16 wakibariki aondoke kwa kuhamishwa bila
kuchukuliwa hatua jambo ambalo limeshangaza wengi wakiwemo Mwenyekiti na Mkurugenzi
wa Halmashauri hiyo.
Airo
pia ameitaka serikali kupitia Wizara ya TAMISEMI kuchua hatua za haraka kumrejesha
Wilayani humo aliyekuwa Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo Bw. Renatus Mtasiwa baada ya kufanya ubadhilifu wa zaidi
ya shilingi milioni 111.7 za Halmashauri hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Mwanza , Mbunge huyo alisema kwamba
kutokana na kitendo cha kuhamishwa kwa aliyekuwa Mweka Hazina Mtasiwa kufanya
ubadhilifu wa fedha za Ruzuku ya shule (Capitation) kiasi cha shilingi milioni
21, fedha za likizo za walimu kiasi cha shilingi milioni 90 kuzichota na
kuzitumia tofauti na ilivyokusudiwa ni wizi ambao anatakiwa kuchukuliwa hatua
kali za kimaadili na kisheria.
Bw.
Airo alisikitishwa na taarifa za Mweka Hazina huyo, ambapo alidai kuwa siku
mbili kabla ya Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Rorya ambacho
kiliketi hivi karibuni nayeye kushindwa kuhudhulia kutokana na kuwa kwenye
majukumu mengine ya Kamati ya Bunge ambapo inadaiwa kuwapatia baadhi ya
madiwani pombe na kuwalewesha kwa siku mbili ili kutomjadili na kuruhusu
ahamishwe kama ilivyoelezwa kwenye kikao hicho.
“Nimesikitishwa
sana na hili suala kwani Mweka Hazina alikuwa anakaimu Nafasi ya Mkurugenzi
akitoka na muda mfupi akifanya ubadhilifu kwa kiwango cha fedha shilingi
milioni 111.7 lakini alichokifanya akaenda kuomba uhamisho Wizarani na sasa
kahamishiwa Hamashauri moja Mkoani Morogoro hivi hili kweli ni halali” alihoji
kwa mshangao .
Aliongeza
kuwa pamoja na kuwepo ubadhilifu huo baadhi ya Madiwani sita (6), Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Rorya Bw. Charles Ochele na Mkurugenzi halmashauri hiyo kwenye
kikao hicho walitaka baraza liazimie kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na
kumtaka arejeshe fedha za Likizo na Walimu alizotafuna lakini baadhi ya
madiwani 16 kati ya 23 walidaiwa kuhongwa na kunyweshwa pombe kuwapinga.
Aidha
Mbunge Airo alisisitiza kuwa suala hilo bado atalivalia njuga hadi kwa Waziri
Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa TAMISEMI Bi Hawa Ghasia ili kumshughulikia
Mweka hazina huyo ikiwa ni pamoja na kumrejesha ili kurudisha fedha alizotafuna
kama alivyo ahidi akijibu maswali ya baadhi ya wabunge waliotaka wezi kwenye
halmashauri wasihamishwe na hata wakihamishwa warudi kujibu tuhuma zao za wizi.
Akizungumzia
suala la Mkuu wa Wilaya Rorya kuwatuhumu moja kwa moja wanasiasa kuwa ndiyo
wanakwamisha ukusanyaji wa makusanyo ya mapato ya Halmashauri ya Wilaya hiyo na
kushuka kwa kiwango kikubwa, alisema kwamba hatua hiyo iliyojitokeza kwenye
Kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Mara (RCC) hivi karibuni ilikuwa na lengo
la kupotosha ukweli kwa wajumbe wa kikao hicho.
Mbunge
Airo alisema taarifa iliyozungumzwa na DC wa Rorya haikuwa na ukweli na
inaonyesha anavyokurupuka kujibu hoja ambazo alipaswa kumachia Mkurugenzi
kuzijibu ambaye ni Mtaalamu na mwenye kuwa na takwimu au hata Mwenyekiti na si
yeye ambaye amekuwa mtu wa kudanganywa na kisha
kuzungumza vyombo vya habari bila utafiti wa kina.
“Nilimsikia
akidai kuwa baadhi ya wanasiasa ndo wamechangia kushuka kwa ukusanyaji wa
mapato ya ndani ya halmashauri kupitia vyanzo vyake na alikwenda mbali
kuwatuhumu wanasiasa bila hata kumshirikisha Mkurugenzi na Mwenyekiti Bw.
Ochele kwani wao ndio walipaswa kujibu au ndiyo walikuwa na majibu sahihi ya
kile kilichopelekea kushuka kwa ukusanyaji huo kwa mwaka wa 2013/2014 ya bajeti
iliyopita.
Alifafanua
kuwa kutokana na kauli hiyo, ameamua kuweka wazi kilichotokea kwenye Jimbo lake
na Halmashauri hiyo kwa kueleza kuwa kwanza amesikitishwa na kauli aliyoitoa DC
huyo ya kuwatuhumu baadhi ya wanasiasa lakini katika makisio ya bajeti ya mwaka
2013/2014 walipanga kukusanya shilingi milioni 615 za ada ya malipo ya kuuza
viwanja, lakini hazikukusanywa na badala yake ilikusanywa shingi milioni
21,293,000/= tu.
“Hapa
malengo hayakufikiwa sasa viwanja havikuuzwa kutokana na Serikali kushindwa
kupeleka kwa wakati fedha ya kulipia fidia kama Halmashauri ilivyoomba huku makusanyo ya ada baada ya kuuzwa viwanja
ikiwa ya maombi ya viwanja hivyo ilikuwa ikusanywe kiasi cha shilingi milioni
12 na badala yake wamepata milioni 92.8”alisema
Aliongeza
kuwa, makusanyo ya kodi za viwanja baada ya kuviuza walitegemea kukusanya
milioni 16 zakini walikusanya shilingi milioni 5, 279,000/= tu sawa na asilimia
33 huku makusanyo ya ambayo ambayo hayakufikiwa ikiwa ni zaidi ya shilingi mia
sita kutokana na kukosekana malipo ya fedha za fidia baada ya kucheleweshwa na
serikali na kupelekea kushuka kwa makusanyo na mapato ya halmashauri hiyo.
Aidha
ushuru wa maegesho ya Pikipiki kuna Kampuni ilipewa zabuni ya kuwa wakala wa
kukusanya ambapo kwa mwezi inawasilisha shilingi 60,000/= jambo ambalo
linashanghaza sana na ukizingatia kuna
kizuizi cha magari na pikipiki ambapo magari makubwa ya mizigo hulipia
shilingi 30,000/= na kufanya chanzo
hicho nacho kushindwa kukusanya vyema mapato ya halmashauri hiyo.
“Hapa
wanasiasa wanahusika vipi kuona mapato yanakusanywa na kampuni iliyopewa zabuni
na kukusanya ushuru chini ya malengo yaliyokusudiwa halafu waheshimiwa madiwani
wanapohoji wanaanza kusakamwa na mkuu wa wilaya kwamba ndo wanasababisha hili
halikubaliki na tunasema mkuu wa wilaya hana weledi wa kuwashambulia wanasiasa
na ache kufanya hivyo” alisisitiza.
Ametoa
wito kwa wananchi kumuunga mkono katika kutetea haki za wana Rorya katika
Halmashauri yao , Lakini pia amemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo kuacha kuwasakama
wanasiasa na kwamba wakati anateuliwa kwenda Wilaya ya Rorya alikuta tayari wao
wamechaguliwa kuwatumikia wananchi na ikizingatiwa wao ni wana rorya hivyo
aache tabia ya kukurupuka kuwasema hovyo na ache mara moja.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.