ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 13, 2014

SUPER STAR WA BONGO MOVIE JB AONGOZA ZOEZI LA UTOAJI FOMU ZA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA NA MAISHA PLUS MWANZA.

Mwigizaji wa filamu za Bongo Jacob Steven aka JB aka Dj Ben, akiwakabidhi akinamama waliofika katika viwanja vya Buhongwa jijini Mwanza kuchukuwa fomu za ushiriki wa shindano la Mama shujaa wa chakula ndani ya Kipindi cha Televisheni cha Maisha Plus kinachotarajiwa kuanza kuruka hivi karibuni kupitia TBC One.
Mmoja kati ya waratibu wa Shughuli za Shirika la Oxfam nchini ambao ni moja kati ya wadhamini wa shindano hilo Mis Jane akigawa fomu kwa vijana waliofika viwanja vya Buhongwa jijini Mwanza kuchukuwa fomu za ushiriki wa shindano la Kipindi cha Televisheni cha Maisha Plus kinachotarajiwa kuanza kuruka hivi karibuni kupitia TBC One.
Babu wa Maisha Plus naye alichagiza kuusu umuhimu wa shindano hilo ambalo msimu huu linakuja likiwa limenogeshwa zaidi huku zawadi zikiboreshwa na kuongezwa hadi kufikia milioni 25. 
Meza kuu na wadau akiwemo Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini (wa pili toka kushoto)

Ni sehemu ya akinamama waliofika katika viwanja vya Buhongwa jijini Mwanza kusikiliza kinachojiri na hatimaye kuchukuwa fomu za ushiriki wa shindano la Mama shujaa wa chakula ndani ya Kipindi cha Televisheni cha Maisha Plus kinachotarajiwa kuanza kuruka hivi karibuni kupitia TBC One.
Meza kuu ikinadi umuhimu wa tukio zima.
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linalenga kuwahamasisha, kuwawezesha na kuwasaidia wanawake na vijana katika sekta ya uzalishaji wa chakula. Mshindi wa msimu wa kwanza (2011) alizawadiwa Power Tiller pamoja na msaada wa kiufundi. Mshindi wa msimu wa pili (2012) alipata zawadi yenye thamani ya shilingi milioni kumi ambayo ameiwekeza kwenye mifugo ya kuku na ujenzi wa kituo cha mafunzo ya kilimo kwa vijana.
"Nitafurahi sana kuona akinamama mnachangamkia fursa hii ambayo licha ya zawadi kuna elimu kubwa ya ujasiliamali ndani yake ambayo mtaipata" says Rahab toka Kivulini Mwanza.
"Kwa kujaza fomu zetu na kushiriki Shindano la Mama Shujaa wa Chakula, umetambua na kuthamini mchango wako binafsi kama mwanamke. unakataa na kuahiadi kutokomeza ukatili wa kijinsia na unajitolea kutetea haki za wanawake kumiliki rasilimali ikiwemo ardhi" says Eluka Kibona toka Oxfam.
Kwa utulivu wakisikiliza yanayojiri ni akinamama wa Mwanza na wadau wengine pichani katika viwanja hivi vya Buhongwa.
Sekta ya habari nayo ilihudhuria tukio hili lenye lengo la kuinyanyua jamii toka anguko la lindi la umasikini.
Ngoma toka Bujora ilisherehesha.
Jamaa alikataa kata kata kuvishwa nyoka begani licha ya kichwa cha nyoka huyo kushikwa barabara na wacheza ngoma wa Bujora.
Dj Ben hakuwa tayari kumweka beganinyoka huyo.....
'Mambo ya Ngoswe mwachie Ngoswe mwenyewe'
Babu wa Maisha plus alishiriki vyema kuhakikisha kila mdau mwenye sifa anapata fomu yake na kuijaza.
"Mie tayari wewe jeh?" says Masai ya Mwanza.
Mtangazaji wa ITV Mwanza Mabere Makubi akihitimisha taarifa yake kupeleka ujumbe kwa walioko majumbani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.