Meneja wa bia ya ndovu, Pamela Kikuli(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (wanaonekana katika picha inayofuata chini) |
BADO mauaji ya tembo hayajapata ufumbuzi wa kudumu nchini Tanzania tangu serikali ya nchi hiyo kusitisha Operesheni tokomeza kutokana na kuwepo madai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu na mauaji ya watu wasio kuwa na hatia.
Kwa mijibu wa taarifa ya Naibu waziri wa Maliasili na utalii nchini Tanzania Lazaro Nyarandu aliyoitoa mwishoni mwa mwaka jana (2013) alidai kuwa idadi ya tembo 60 wameuawa katika kipindi cha miezi miwili tu ya mwezi Novemba na Disemba ikilinganishwa na tembo wawili tu waliouawa mwezi mwa kumi mwaka huu.
Hata hivyo idara za ulinzi zilikubaliana kuwaua majangili watakaobainika wakiwaua tembo hao kipindi ambacho msako huo ulikuwa ukiendelea mwezi Oktoba mwaka huu
Hata hivyo serikali ilisitisha operesheni hiyo kufuatia malalamiko kwamba watekelezaji wa msako huo walikuwa wakikiuka haki za binadamu.
Waziri mkuu wa Tanzania alikaririwa akisema operesheni hiyo ilikuwa na nia njema lakini taarifa za kuwepo vitendo vya mauaji na ukikwaji wa haki za binadamu ndicho ambacho hakikubaliki na serikali
Hata hivyo matokeo ya uchunguzi wa kamati maalumu kuhusiana na kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu ndiyo uliosababisha Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwafukuza kazi mawaziri ,Shamsi Vuai Nahodha wa Jeshi la Ulinzi, Emmanuel Nchimbi wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Utalii na Maliasili Khamis Kagasheki na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo David Mathayo.
Nchi za kutoka bara la Asia ndizo zinazodaiwa kujihusisha Zaidi na biashara ya pembe za ndovu hali inayoongeza kasi ya ujangili na mauaji ya tembo nchini Tanzania.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.