MWANZA.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Mbaraka Abduwakili amewataka wajumbe wa Baraza kuu la Taifa Idara ya Uhamiaji nchini kujikita zaidi kujadili utendaji kazi wa watumishi wa Idara hiyo.
Kufanya thathimini ya utendaji wa watumishi ambao baadhi yao wamekaa muda mrefu kwenye vituo vyao vya kazi na kuzoeana hali ambayo imedaiwa na kudhaniwa kuwa inazorotesha ufanisi wa majukumu ya kila siku na hata huduma kutolewa kwa wageni na wananchi bila kukidhi ubora wa maadili ya viapo vya kazi.
Kufanya thathimini ya utendaji wa watumishi ambao baadhi yao wamekaa muda mrefu kwenye vituo vyao vya kazi na kuzoeana hali ambayo imedaiwa na kudhaniwa kuwa inazorotesha ufanisi wa majukumu ya kila siku na hata huduma kutolewa kwa wageni na wananchi bila kukidhi ubora wa maadili ya viapo vya kazi.
Akifungua Mkutano mkuu wa Baraza hilo jana Jijini Mwanza , alisema kwamba baadhi ya askari na watumishi wa Wizara yake wanadaiwa kukaa muda mrefu sehemu moja ikiwa ni kwenye vituyo vyao vya kazi jambo ambalo linachangia baadhi yao kushindwa kutekeleza majukumu yao na kujihusisha na ulevi na vitendo ambavyo haviruhusiwi na kuzorotesha ufanisi wakati wa utowaji huduma.
Abduwakili alisema kwamba mazoea ya watumishi hao wa Idara zilizo chini ya Wizara yake ni vyema wakazingatia viapo vya utendaji wao wa kazi na kujikita kutoa huduma kwa ufanisi zaidi kwani hata solidalite yao inasema kwamba masilai bora kwanza lakini pia utendaji bora wa kazi.
Abduwakili aliwataka wajumbe 130 ambao ni wawakirishi wa watumishi na viongozi wa vyama vya wafanyakazi katika Idara za Uhamiaji kutoka Mikoa yote nchini kuzingatia kujadili uboreshwaji wa utendaji kazi zaidi pamoja na kuweka mapendekezo ya kuboreshewa masilahi yao lakini wawafikishie ujumbe wa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwenye vituo vyao vya kazi.
“Askari au mtumishi wa serikali akikaa muda mrefu kwenye kituo chake na kuzoeana mazingira na watu ambao anawajibika kuwapatia huduma hujikuta wakiharibu na kurubunika na kufanya vitendo visivyoendana na viapo vyao vya kazi ikiwa ni pamoja na miiko ya maadili ya utumishi wa umma, na wengine kuwa walevi” alisema na kuongeza kuwa.
Aidha amewataka wajumbe wa mabaraza ya wafanyakazi na viongozi wa vyama vya wafanyakazi (TUGHE) msikubali kuwatetea watumishi walevi na wanaoharibu kazi kwa vitendo vya rushwa jambo ambalo huzpunguza uaminifu wa Idara hii kwa Umma na kuzorotesha utendaji wa Idara hii mhimu ,badala yake muwe watetezi wa watumishi wanotenda kazi zao kwa uadilifu na ufanisi mkizingatia masilahi ya taifa kwanza.
Awali Kwa upande wake Kamishina Mkuu wa Idara ya Uhamiaji nchini Sylivester Ambokile akimkaribisha Katibu Mkuu Abduwakili alisema lengo la Mkutano huo wa Baraza kuu ni kujadili changamoto mbalimbali za watumishi kwa kushirikiana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi (TUGHE) pamoja na masilahi ikiwa ni pamoja na uboreshwaji wa Idara kupata kutekeleza majukumu kwa ufanisi zaidi.
Ambokile alisema kwamba Mkutano huo hufanyika kila mwaka ikiwa ni utangulizi kabla ya kikao cha watendaji wa Idara hiyo kutoka Mikoa yote ya kujadili na kuweka mikakati ya utekelezwaji wa sera na utolewaji wa huduma kwa wananchi na wageni hapa nchini hali ambayo huwapatia fursa zaidi ya kuzipitia changamoto zilizopo na zinazojitokeza kwenye utekelezaji wa kila siku wa majukumu ya idara hiyo.
“Tunapokutana kwanza ni kubadilishana uzoefu, pili ni kuzitazama na kuweka mikakati ya kupambana na changamoto mbalimbali kasha kutoka na maazimio ya utekelezaji wake pamoja na kuangalia masilahi ya watumishi kulingana na mazingira yaliyopo kwenye vituo vyao vya kazi na hata kuweka mikakati ya kuitekeleza kwa ufanisi zaidi na kushughulikia yale yanayotakiwa ikiwa kufikishwa kwetu viongozi na watendaji wakuu Wizarani” alisema.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha watumishi Serikali kuu na Afya (TUGHE) Taifa John Sanjo ameitaka serikali, kuacha kuwagawa wafanyakazi na badala yake wazingatie Walaka wa 2013 wa watumishi kama Katiba inavyoelekeza, kufatia kuwepo baadhi ya watendaji na waajili kutowaruhusu baadhi ya wakuu kushiriki katika vikao vya kutunga sera .
“Tayari serikali imeisha jichanganya, inataka kuwagawa kwa jambo moja la kuwa kuwa na vyama vingi,ambapo hata Katiba ya nchi inasema kila mwananchi anayo haki ya kushiriki na anao wajibu wa kuchagua chama anachokitaka hata sheria ya ajira na mahusiano kazini inasema hivyo isipokuwa vyombo vya ulinzi tu sheria ndogo inasema wanacha wa TUGHE wanatakiwa kushiriki katika kutunga sera” alisisitiza.
Sanjo alisema kuwa mfano ni Katibu Mkuu wa Wizara, lakini kuna walaka uliotolewa na Wizara ya Menejimenti na Utumishi wa Umma kwa waajili kuwa kiongozi wa Chama akiwa mtumishi kwenye eneo lake haruhusiwi kuingia katika kikao cha kutunga sera na tayari wameelekezwa kuondolewa na kudhuhiliwa kushiriki hili ni kukosa na wameamua hata mkuu wa madereva asiwe mwanachama.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.