ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 27, 2014

MAKONGORO NA RAFIKI ZAKE WASHEREHEKEA MWAKA MPYA KWENYE KITUO CHA KULEA WAZEE.

Juma Makongoro ambaye Mkuu wa Doria za Uvuvi Kanda ya Mwanza akimkumbatia mama mmoja kati ya wazee wa Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambapo yeye pamoja na rafiki zake wakiwemo wengine toka sekta ya uvuvi pamoja na wafanyabiashara walitembelea kituo hicho kwaajili ya kula pamoja na kutoa misaada kama sehemu ya kusherehekea mwaka mpya 2014.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bernard Polycap akizungumza na wazee wa Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambapo yeye aliwaasa wazee hao kuunda vikundi  kwa kuzingatia vipaji vyao na kujiorodhesha ili ofisi yake itizame jinsi ya kuwawezesha mitaji midogo midogo itakayo wasaidia kuanzisha miradi ya kujikimu kwa mahitaji binafsi.


Juma Makongoro ambaye Mkuu wa Doria za Uvuvi Kanda ya Mwanza (kulia) akimkabidhi msaada wa nguo Bi.Angelina Jonas katika sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya 2014 iliyofanyika katika Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza. Kushoto ni Mkurugrnzi wa kituo hicho. 
Makabidhiano yakiendelea katika kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza, ambapo zawadi za nguo, mafuta, sabuni, mchele, unga na bidhaa nyinenezo gawiwa kwa mabalozi wa wazee hao ambapo kila balozi anakaa na watu wake kisha wana gawana kwa usawa.
Mratibu wa ziara hafla hiyo Juma Makongoro (kushoto) akiwa na mkurugenzi wa kituo wakisaidiana kugawa vinywaji kwa wazee wa Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Wazee wengi waliopo kwenye kituo hiki waliathiriwa na ugonjwa wa ukoma, upofu na wengine ni walemavu kutokana na ajali na majanga mbalimbali yaliyowakumba kwenye jamii zao hivyo kuwatembelea imekuwa ni faraja sana kwao. 
Marafiki wa Juma Makongoro kutoka Forum Syd nao waliungana naye kuleta zawadi zao na kujumuika pamoja kwenye sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya.
Juma Makongoro ambaye ni Mkuu wa Doria za Uvuvi Kanda ya Mwanza akizungumza na wazee wa Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Kusanyiko la wadau ndani ya ukumbi wa sherehe.
Akina mama ambao ni marafiki wa Makongoro wakimtunza fedha mama huyu ambaye kutokana na kupatwa na ugonjwa wa ukoma siku za nyuma (sasa amepona) napata shida sana kujihudumia kwani kwa sasa hana viganja na amekatwa mguu mmoja. 
Wazeee na walemavu wasio jiweza wa Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande wakisubiri zamu ya kugawiwa zawadi.
Serikali ambayo ndiyo yenye jukumu la kuwatunza na kuwalea wazee hawa kwa mahitaji ya chakula, mavazi na huduma nyingine muhimu kama umeme na maji ni kama imewatelekeza kwani tangu mwezi wa 5 mwaka jana 2013 serikali  inadaiwa kwani haija peleka msaada wowote wa chakula kukihudumia kituo hadi leo.
Hivyo wazee hao wanaishi katika maisha magumu wakitoroka kambini hapo na kuzama mijini na kugeuka kuwa omba omba.

KITUO NA IDADI YA WATU:-
 Wazee wanaume 60.
Wazee wanawake 96.
Vijana wa kiume 54.
Vijana wa kike 55.
Watoto wa kiume 40.
Watoto wa kike 40.
Pamoja na dhima ya Serikali kukitenga kituo hiki cha Kalwande kuwa mahususi kulea wazee na walemavu wasio jiweza changamoto nyingine inajitokeza hapa, watoto wanazaliwa nao wanakuwa na kufikia umri mkubwa nao wana pata watoto kwa hiyo kituo kinakuwa si cha kuwalea wazee pekee bali kuwalea watoto pia ambao wanakabiliwa na changamoto ya kukosa elimu na malezi sahihi wakidhani maisha ni kuomba omba. 
Kikundi cha ngoma cha Kwaya ya Mt. Cecilia kilitumbuiza na hapa marafiki walijumuika na wazee pamoja na watoto wa kituo hicho kusakata ngoma kama sehemu ya kusherehekea mwaka mpya 2014.
Akiwakilisha Ma-blogger  G. Sengo naye hakusita kuhusika pale kati.
Angelina Jonas ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyekimbilia kituoni hapa kupata hifadhi marabaada ya kupata misukosuko toka kwenye jamii aliyokuwa akiishi yeye ni mfanyabiashara wa maandazi na amekuwa akiifanya shughuli hii kwaajili ya kujipatia fedha za kujikimu na mahitaji madogo madogo, licha ya changamoto nyingi zinazo mzunguka.
Naye mama Maria Petro ana duka lake la kuuza bidhaa mchanganyiko kama kanga, vitenge, unga, mchele na maandazi  hapa akimpatia huduma mteja wake bi. Jetruda Mwidima (kulia) ambaye anatatizo la kuanguka anguka kwenye moto. 
Picha ya pamoja ya kamati ya wadau walio fanikisha sherehe hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.