Mwanza
MARA mabingwa mbio za mitumbwi kanda ya Ziwa.
KIKUNDI wapiga kasia Wanaume kinachoongozwa na nahodha Benedicto Chamba kutoka Mkoa wa Mara kimetwaa ubingwa wa Kanda ya Ziwa wa mashindano ya mbio za Mitumbwi zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia nchini kupitia Bia ya Balimi Extra Lager na hivyo kujitwalia zawadi ya fedha taslimu Shilingi 2700,000/=,Kikombe pamoja na medali za dhahabu.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Eliud Prosper kutoka Gagera ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 230,000/=,nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Toto Benedicto kutoka Ukerewe ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 1700,000/=,nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha nahodha JJ. Buda kutoka Mara ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 900,000/=na nafasi ya tano hadi kumi walipewa kufuta jasho cha silingi 400,000/= kila kikuni ambao ni kikundi cha nahodha Totoji Mazige kutoka Ukerewe,kikundi cha Constantine Lusalago kutoka Mwanza, kikundi cha Bernard Charles kutoka Mara,kikundi cha Lenard Zungu Mwanza,kikundi cha Daniel Mugenda Mwanza na kikundi chaSimon Fundi kutoka Ukerewe.
Upande wa Wanawake kikundi cha nahodha Regina Kazungu kutoka Jijini Mwanza walitwaa Ubingwa wa Kanda ya Ziwawa mashindano hayo na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 2300,000/=,kiombe pamoja na medali za dhahabu.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Nyamizi Deo kutoka Musoma ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 1700,000/=,nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Jenifaer Elias kutoka Ukerewe,nafasi ya nne ilikwenda kwa kikundi cha nahodha Muhate Mwocha kutoka Ukerewe na nafasi na tano hadi kumi walizawadiwa kifuta jasho cha fedha taslimu shilingi 250,000/=
Meneja mauzo na usambazaji wa TBL Kanda ya Ziwa, Maalaki Sitaki aliwapongeza washiriki wote tangu mashindano hayo yalipoanza kwangazi ya mikoa hadi Kanda yamekuwa ya amani nautulivu lakini pia aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2013 na kuwaomba wakautumie vizuri ubingwa wao kwa maandailizi ya mashindao hayo mwakani na wakawe mabalozi wazuri wa bia ya Balimi Extra Lager.
Nae mgeni rasmi, Meya wa manispaa ya jiji la Mwanza kwa niaba ya Mkoa Inginia Evaristo Ndikilo, Stanslaus Mabula, aliipongeza TBL, kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo kwani kupia mashindano hayo ni mchango mkubwa sana kwa jamii na kwa Serikali inalitambua hilo na iko pamoja na TBL kusaidia pale itakapo hitaji msaada.
Mwisho mabula aliwapongeza mabingwa wote na kuwatakia kusherekea ubingwa wao kwa amani na pia aliwataka wakawe mabalozi wazuri wa bia ya balimi extra lager ili wadhamini waendelee kudhamini mashindano hayo.
Fainali za mashindano yam bio za mitumbwi zilihusisha Mkoa wa Kigoma, Kagera, Mwanza ,Mara na Kisiwa cha Ukerewe ambacho pia hubeba hadhi ya Mkoa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.